Waebrania 10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 BASSI kwa kuwa torati ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo, kwa dhahihu zile zile wanazozitoa killa mwaka daima, hawawezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao. 2 Kama wangeweza, wangeacha kuzitoa; kwa maana waabuduo, walipokwisha kusatishwa kwa marra moja, wasingejiona tena kuwa na dhamhi? 3 Lakini katika hizo liko kumbukumbu la dhambi killa mwaka. 4 Maana haiyumkini damu ya mafahali na mbuzi iondoe dhambi. 5 Kwa biyo ajapo ulimwenguni, anena, Dhambi na toleo hukutaka, lakini mwili uliniwekea tayari: 6 Kafara na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo: 7 Ndipo nilisema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) niyafanye mapenzi yako, Mungu. 8 Hapo juu anenapo, Dhabihu na matoleo na kafara na sadaka za dhamhi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo ilivyoamuru torati), 9 ndipo alinena, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, illi kusudi alisimamishe la pili. 10 Katika mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo marra moja. 11 Na killa kuhani husimama killa siku akifanya ibada, akitoa dhabihu zilezile marra nyingi; nazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi. 12 Lakini huyu, alipokwisha kutoa dhabihu nioja kwa dhambi, idumuyo hatta milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu; 13 akingojea hatta adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake. 14 Maana kwa toleo moja amewakamilisha hatta milele wanaotakaswa. 15 Na Roho Mtakatifu yatushuhudia; kwa maana, baada ya kunena, 16 Hili ni agano nitakalowapa baada ya siku zile, anna Bwana, Nitatia sharia zangu mioyoni mwao, na katika akili zao nitaziandika; ndipo anenapo. 17 Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa. 18 Bassi ondoleo la baya lilipo, hapana toleo tena kwa dhambi. 19 Bassi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, 20 njia aliyotuanzia mpya, hayi, ipenyayo katika pazia, yaani mwili wake; 21 na Kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu; 22 tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa mwili kwa maji safi. 23 Tulishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni amini; 24 tukaangaliane kiasi cha kusukumana katika upendo na kazi nzuri; 25 tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tukionyana; na tukizidi, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia. 26 Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; 27 bali kuitazamia hukumu kwenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao. 28 Mtu aliyeidharau sharia ya Musa, alikufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu. 29 Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa nayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho ya neema? 30 Maana twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake. 31 Ni jambo la kutisba kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hayi. 32 Lakini zikumbukeni siku za kwanza, ambazo, mlipokwisha kutiwa nuru, mlistahimili mashindano makubwa ya maumivu; 33 pindi mlipotwezwa kwa mashutumu na mateso, na pindi mliposhirikiana na wale waliotendewa hayo. 34 Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika mafungo, mkakubali kwa furaba kunyangʼauywa mali zenu, mkijua nafsini mwenu kwamba mna mali mbinguni iliyo njema zaidi, idumnyo. 35 Bassi msiutupe njasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu. 36 Maana mnahitaji uvumilivu, illi mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu muipate abadi. 37 Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajae atakuja, wala hatakawia. 38 Lakini mwenye haki ataishi kwa imani; nae akisitasita, roho yangu haina furaha nae. 39 Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali miongoni mwao walio na imani ya kutuokoa roho zetu. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania