Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waebrania 1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 KWA sehemu nyingi na kwa namna nyingi Mungu zamani alisema na babu zetu katika manabii,

2 mwisho wa siku bizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi yote, kwa yeye aliufanya ulimwengu.

3 Yeye kwa kuwa ni mwanga wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivitengeneza vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya peke yake utakaso wa dhambi zetu, aliketi juu mkono wa kuume wa ukuu;

4 amefanyika bora sana kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko wao.

5 Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Mwana wangu ndiwe, mimi leo nimekuzaa? na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, na yeye kwangu mwana?

6 Hatta amletapo tena mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, anena, Na malaika wote wa Mungu wamsujudu.

7 Na katika khabari za malaika anena, Afanyae malaika zake kuwa pepo, na watumislii wake ndimi za moto.

8 Lakini katika khabari ya Mwana anena, Kiti chako, Mungu, ni cha milele; na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya kunyoka.

9 Umependa haki, umechukia maasi: kwa sababu hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, mafuta ya shangwe kupita wenzako.

10 Na, wewe, Bwana, mwanzo umeitia misingi ya inchi, na mbingu ni kazi za mikono yako;

11 hizi zitaharibika, na wewe hukaa; hizi zitachakaa kama nguo,

12 na kama mavazi utazizinga, nazo zitabadilika; lakini wewe u yeye yule, na miaka yako haitakoma.

13 Je! yuko malaika aliyeambiwa nae maneno haya wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume hatta nitakapoweka adui zako chiui ya nyayo zako?

14 Hawo wote si roho zitumikazo, wakitumwa kuwakhudumu wale watakaourithi wokofu?

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo