Ufunuo 3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 NA kwa malaika wa kanisa lililo katika Sardi, andika; Haya ayanena yeye aliye nazo roho saba za Mungu na zile nyota saba: Najua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hayi, nawe umekufa. 2 Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe manibo yaliyosalia, yaliyo tayari kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu. 3 Bassi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Illakini usipokesha nitakuja kwako kama mwizi, nawe hutaijua saa nitakayokuja kwako. 4 Lakini unayo majina machache, hatta katika Sardi, watu wasioyatia uchafu mavazi yao. Nao watakwenda pamoja nami katika mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili. 5 Yeye ashindae atavikwa mavazi meupe, wala sitalifuta jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitaliungama jina lake mbele za Baba yaugu, na mbele ya malaika zake. 6 Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. 7 Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Filadelfia andika; Haya ayanena yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daud, mwenye kufungua wala hapana afungae, nae afunga wala hapana afuuguae. 8 Najua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, wala hapana awezae kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe ulilitunza neno langu, wala hukulikana jina langu. 9 Tazama, nakupa walio wa sunagogi la Shetani, wasemao kwamba wao ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uwongo. Tazama, nitawafanya waje wasujudu mbele ya miguu yako na kujua ya kuwa nimekupeuda. 10 Kwa kuwa ulilishika neno la uvumilivu wangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kujaribiwa iliyo tayari kuujia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya inchi. 11 Tazama, naja upesi. Shika sana ulicho nacho asije mtu akaitwaa taji yako. 12 Yeye ashindae, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, Yerusalemi ulio mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya. 13 Yeye aliye na sikio na asikie neno bili ambalo Roho ayaambia makanisa. 14 Na kwa Kanisa lililo katika Laodikia andika; Haya ayanena yeye aliye Amin, Shahidi aliye mwaminifu, mwanzo wa viumbe vya Mungu. 15 Najua matendo yako, ya kuwa huwi baridi wala hu moto; ingekuwa kheri kama ungekuwa baridi au moto. 16 Bassi, kwa sababu una uvuguvugu, wala huwi baridi wala moto, nitakutema kama mate katika kinywa changu. 17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u maskini, na mtu wa kuhurumiwa, na mhitaji, na kipofu, na nchi. 18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri; na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya nchi wako isionekane; na dawa ya macho ya kujipaka macho yako upate kuona, 19 Mimi nawakemea wote niwapendao, na kuwarudi: bassi uwe na bidii, ukatubu. 20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha: mtu akiisikia sauti yangu na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nitakula pamoja nae, na yeye pamoja nami. 21 Yeye asbindae, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda, nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. 22 Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania