Ufunuo 21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 NIKAONA mbingu mpya na inchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na inchi za kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. 2 Nami Yohana nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemi mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. 3 Nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wana Adamu, nae atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Na Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, Mungu wao. 4 Nae atafuta killa chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena: wala maombolezo, wala kilio, wala taabu haitakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. 5 Na yeye aketiye juu ya kiti cha enzi akasema, Tazama, nafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika, kwa maana haya ni maneno ya kweli, na ya uaminifu. 6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa mwenye kin maji ya chemchemi ya maji ya uzima, burre. 7 Yeye ashindae atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, nae atakuwa Mwana wangu. 8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, nae waabuduo sanamu, na wawongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili. 9 Akaja mmoja wa wale malaika saba walio na vichupa vile saba vijaavyo yale mapigo saba ya mwisho, akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi arusi, mke wa Mwana kondoo. 10 Akanichukua katika Roho hatta mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemi, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyiezi Mungu, 11 wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi safi, kama bilauri: 12 ulikuwa ua ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango thenashara, na katika ile milango malaika thenashara, na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila thenashara za wana wa Israeli. 13 Upande wa mashariki milango mitatu: na upande wa kaskazini milango mitatu; na upande wa kusini milango mitatu: na upande wa magharibi milango mitatu. 14 Na ukuta wa mji una misingi thenashara, na katika ile misingi majina theriashara ya mitume wa Mwana kondoo. 15 Na yeye aliyenena nami alikuwa na mwanzi wa dhababu apate kuupima mji na milango yake na ukuta wake. 16 Na ule mji ni wa mrabba, na marefu yake sawa sawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi, hatta stadio thenashara elfu. Marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake mamoja. 17 Akaupima ukuta wake, ni dhiraa misi na arubaini na nne, kwa kipimo cha mwana Adamu, maana yake, cha malaika, 18 Na majenzi ya nle ukuta ya yaspi, na mji ule dhahabu safi, mfano wa kioo safi. 19 Na misingi ya ukuta wa mji imepambwa kwa killa jito la thamani. Msingi wa kwanza yaspi; wa pili sapfiro; wa tatu kalkedo; wa nne smaragdo; 20 wa tano surdonuksi; wa sita sardio; wa saba krusolitho; wa nane berullo; wa tissa topazio; wa kumi, krusopraso; wa edashara huakintho; wa thenashara amathusto. 21 Na milango thenashara, lulu thenashara: killa mlango ni lulu moja. Na njia ya mji dhahabu safi kama kioo kisichoizuia nuru. 22 Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyiezi ni hekalu lake, na Mwana kondoo. 23 Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi uuangaze, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana kondoo. 24 Na mataifa wa hao wanaookolewa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa inchi wataleta utukufu wao na heshima yao ndani yake. 25 Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku. 26 Na wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake. 27 Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyae machukizo na uwongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania