Ufunuo 20 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 NIKAONA malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa abuso, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. 2 Akamshika joka, yule nyoka wa zamani, aliye msingiziaji, Shetani, akamfunga miaka elfu, 3 akamtupa katika abuso, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hatta ile miaka elfu itimie; na baada ya haya imepasa afunguliwe muaa mchache. 4 Nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, wakapewa hukumu: nikaona roho zao waliokatwa kichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia nyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea alama yake katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; wakawa hayi, wakamiliki pamoja na Kristo miaka elfu. 5 Na wafu waliosalia hawakuwa hayi, hatta ikatimia ile miaka elfu. Huo ndio ufufuo wa kwanza. 6 Yu kheri, mtakatifu, aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watamiliki pamoja nae miaka elfu. 7 Na ile miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa atoke kifungoni mwake: 8 nae atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za inchi, Gog na Magog, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. 9 Wakapanda juu ya upana wa inchi, wakazinga kituo chta watakatifu, na mji uliopendwa. Moto ukashuka katika mbingu kutoka kwa Mungu, ukawala. 10 Na yule Msingiziaji, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule nyama na yule nabii wa nwongo. Na wataumwa mchana na usiku hatta milele na milele. 11 Nikaona kiti eba enzi, cheupe, kikubwa, nae aketiye juu yake; inchi na mbingu zikakimbia nso wake, na mahali pao hapakuonekana. 12 Nikawaona wafu, wakubwa na wadogo, wamesimama mbele za Mungu; vitabu vikafunuliwa. Kitabu kingine kikafunuliwa, kilicho eha uzima, wafu wakahukumiwa kwa mambo ya matendo yao. 13 Bahari ikawatoa wafu waliomo ndani yake. Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu walio ndani yake. Wakahukumiwa killa mtu kwa kadiri ya matendo yao. 14 Mauti na Kuzimu wakatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili. 15 Na ikiwa mtu hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania