Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ufunuo 2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 KWA malaika wa kanisa lililo katika Efeso andika; Haya ayanena yeye azishikae nyota saba katika mkono wake wa kuume, aendae kati kati ya vile vinara saba vya dhahabu.

2 Najua matendo yako, na taabu yako, na uvumilivu wako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa wawongo;

3 tena ulistahimili na kuwa na uvumilivu, na kwa ajili yangu umejitaabisha wala hukuchoka.

4 Lakini nina neno jun yako, kwa sababu umeacha npendo wako wa kwanza.

5 Bassi, kumbuka ulikoanguka, nkatubu, ukayatende matendo ya kwanza. Lakini, usipotenda hivyo, naja kwako upesi, nitaondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.

6 Lakmi unalo neno hili kwamba wayachukia matendo ya Wanikolaiti, niyachukiayo na mimi.

7 Yeye alive na sikio, na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindae, nitampa kula matunda ya mti wa uzima ulio kati kati va bustani ya Mungu.

8 Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Smurna andika; Haya ayanena yeye aliye wa kwanza na wa mwisbo, aliyekuwa amekufa, akawa hayi.

9 Najua matendo yako na mateso yako na umaskini wako (lakini u tajiri), na matukano yao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sunagogi la Shetani.

10 Usiogope mambo yatakavokupata: tazama mshitaki atawatupa baadhi yenu gerezani illi mjaribiwe, nanyi mtakuwa na mateso siku kumi. Uwe mwaminifu hatta kufa, nami nitakupa taji ya uzima.

11 Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindae hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.

12 Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Pergamo, andika; Haya ayanena yeye aliye na upanga mkali, mkali kuwili;

13 Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha Shetani: nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hatta katika siku za Antipa shahidi wangu mwaminifu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.

14 Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaam, yeye aliyemfundisha Balak atie ukwazo mbele ya wana wa Israeli, wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.

15 Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolaiti, niyachukiayo.

16 Tubu; na usipotubu naja kwako upesi, nitafanya vita juu yako kwa upanga wa kinywa changu.

17 Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindae nitampa kula baadhi ya ile manna iliyofiehwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina, jina asilolijua mtu illa yeye aliyepewa.

18 Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Thuatera andika, Haya ayanena Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho kama mwako wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.

19 Najua matendo yako na upendo wako na khuduma yako na uaminifu wako na uvumilivu wako na matendo yako; tena matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.

20 Lakini nina maneno machache juu yako, ya kwamba wamwacha yule mwanamke Yezebel, yeye ajiitae nabii, nae awafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, illi wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.

21 Nami nimempa muda illi atubu uzinzi wake, nae bataki kutubu.

22 Tazama, nitumtupa juu ya kitanda, na hawo wazinio pamoja nae, wapate mateso makubwa wasipotubu matendo yao;

23 nami nitawaua watoto wake kwa manti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzae viuno na mioyo. Nami nitampa killa mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yenu.

24 Lakini nawaambia ninyi, nao wengine walio katika Thuatera, wo wote wasio na mafundisho haya, wasiozijua fumbo za Shetani kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yen umzigo mwungine.

25 Illa mlicho nacho kishikeni, hatta nitakapokuja.

26 Na yeye ashindae na kuyatunza matendo yangu hatta mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,

27 nae atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyangi visetwavyo, kama mimi nilivyopokea kwa Baba yangu.

28 Nami nitampa nyota ya assubuhi.

29 Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo