Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ufunuo 17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 AKAJA mmoja wa malaika wale saba wenye vile vichupa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi,

2 ambae wafaime wa inchi walizini nae, nao wakaao katika inchi wakalevywa kwa mvinyo ya uasharati wake.

3 Akanichukua katika Roho hatta jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu va nyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya ukafiri, mwefiye vichwa saba na pembe kumi.

4 Na mwanamke yule alikuwa ameliwa nguo ya porfuro, na nyekuudu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, mwenye kikombe cha dhahabu mkononi mwake kilichojawa na machukizo na machafu ya uasharati wake,

5 Na katiksi kipaji cha uso wake alikuwa na jina, limeandikwa, SIRI, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAILABA NA MACHUKIZO YA INCHI.

6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.

7 Na yule malaika akaniambia, Kwani kustaajabu? Nitakuambia siri ya mwanamke huyu, na ya nyama amehukuae, mwenye vile vichwa saba na zile pemhe kumi.

8 Yule nyama uliyemwona alikuwako, nae hayuko, nae yu tayari kupanda katika abuso na kwenda kwenye uharibifu. Nao wakaao juu ya inchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watataajabu wamwonapo yule nyama, ya kwamba alikuwako, nae hayuko, nae atakuwako.

9 Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke yule.

10 Navyo ni wafalme saba. Watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. Nae atakapokuja imempasa kukaa muda mchache.

11 Na yule nyama aliyekuwako nae hayuko, yeye ndiye wa nane, nae ni mmoja wa wale saba, nae aenenda kwenye uharibifu.

12 Na zile pemlbe kumi ulizoziona ni wafalme, ambao hawajaupokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme kwa saa moja pamoja na yule nyama.

13 Hawa wana shauri amoj, nao wampa yule nyama nguvu zao na mamlaka yao.

14 Hawa watafanya vita na Mwana kondoo, na Mwana kondoo atawashinda, kwa maana ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme; nao walioitwa wateule, waaminifu, watashinda pamoja nae.

15 Akaniambia, Yale maji uliyoyaona, aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.

16 Na zile pembe kumi ulizoziona juu ya nyama, hao watamchukia yule kahaba, na watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kahisa kwa moto.

17 Maana Muugu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule nyama ufalme hatta maneno ya Mungu yatimizwe.

18 Na yule mwanamke uliyemwona, ndiye mji ule mkubwa, mwenye ufalme juu ya wafalme wa inchi.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo