Ufunuo 16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 NIKASIKIA sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Enendeni, mkavimimine vile vichupa vya ghadhabu ya Mungu juu ya inchi. 2 Akaenda wa kwanza, akakimimina kichupa chake juu ya inchi, pakawa jipu baya, ovu, juu ya wale watu wenye alama ya nyama, na wale wenye kuisujudu sanamu yake. 3 Malaika wa pili akakimimina kichupa chake juu ya bahari, pakawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho va uhayi vikafa katika bahari. 4 Malaika wa tatu akakimimina kichupa chake juu mito, na chemchemi za maji, zikawa damu. 5 Nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, ee Bwana, ulioko, uliyekuwako, mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivu; 6 kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na manabii, nawe umewapa damu, wainywe; nao wamestahili. 7 Nikaisikia madhbahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyiezi, za kweli, za haki hukumu zako. 8 Malaika wa nne akakimimina kichupa chake juu ya jua; likapewa kuwaunguza wana Adamu kwa moto. 9 Wana Adamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo yote, wala hawtikutubu na kumpa utukufu. 10 Malaika wa tano akakimimina kichupa chake juu ya kiti cha enzi cha yule nyama, ufalme wake ukatiwa giza, wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu yao, 11 wakamtukana Mungu wa mbingu kwa sababu ya maumivu yao, na kwa sababu ya majipu yao, wala hawakuyatubia matendo yao. 12 Malaika wa sita akakimimina kichupa chake juu ya mto ule mkubwa Eufrate, maji yake yakakauka illi njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua. 13 Nikaona roho tatu za uchafu kama vyura zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule nyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uwongo. 14 Maana udizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa inchi na wa ulimwengu wofe, kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyiezi. 15 Tazama, naja kama mwizi. Yu kheri akeshae, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi wakaone aibu yake. 16 Akawakusanya hatta maliali paitwapo kwa Kiebrania, Armageddon. 17 Malaika wa saba akakimimina kichupa chake katika hewa. Sauti kuu ikatoka katika hekalu ya mbinguni, kalika kiti kile cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa. 18 Pakawa sauti na radi na umeme, na palikuwa tetemeko la inchi, kubwa, ambalo tangu wana Adamu kuwako juu ya inchi halikuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo. 19 Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ilianguka: na Babeli ule mkuu nkakumbukwa mbele za Mungu, ampe kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake. 20 Killa kisiwa kikakimbia, na milima haikuonekana tena. 21 Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kuloka mbinguni juu ya wana Adamu. Wana Adamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe. Maana pigo lake kubwa mno. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania