Ufunuo 14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 NIKAONA, na tazama, Mwana kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arubaini na nne elfu pamoja nae, wenye jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao. 2 Nikasikia sauti kutoka mbinguni kama santi ya maji mengi na kama sauti ya radi kuu. Nikasikia sauti ya wapiga vinubi, wakivipiga vinubi vyao: 3 nao waimba wimbo niliouona kuwa mpya mbele ya kili cha enzi, na mbele ya wale nyama wane wenye uhayi, na wale wazee; na hapana mtu aliyeweza kujifunza uimbo ule illa wale mia na arubaini na nne elfu walionunuliwa katika inchi. 4 Hawa udio wasiotiwa najis pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana kondoo killa aendako. Hawa walinunuliwa katika inchi, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana kondoo. 5 Na katika vinywa vyao haikuonwa bila. Maana hawana mawaa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. 6 Nikaona malaika niwingine akiruka kati kati ya mbingu, mwenye injili ya milele, awakhubiri wakaao juu ya inchi na killa taifa na kabila na lugha na jamaa, 7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, kamtukuzeni, maana saa ya hukumu yake imekuja. Kamsujuduni yeye aliyezifanya mbingu na inchi na bahari na chemchemi za maji. 8 Malaika mwingine akamfuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya hasira ya uasharati wake. 9 Malaika wa tatu akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu akimsujudu nyama na sanamu yake, na kupokea alama katika kipaji cha uso wake au katika mkono wake, 10 yeye nae atakunywa mvinyo ya hasira ya Mungu iliyotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji katika kikombe cha ghadhabu yake, nae ataumwa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika walakalifu na mbele za Mwana kondoo. 11 Na moshi wa maumivu yao wapanda juu hatta milele na milele, nao bawana raha mchana na usiku, bao wamsujuduo nyama na sanamu yake, na killa aipokeae alama ya jina lake. 12 Hapo ndipo penye uvumilivu wa watakatifu wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu. 13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Wa kheri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; na matendo yao yafuatana nao. 14 Nikaona, na tazama, wingu jeupe, na juu ya wingu hilo ameketi mmoja, mfano wa Mwana Adamu, mwenye taji ya dhahabu juu ya kichwa chake, na katika mkono wake mundu mkali. 15 Malaika mwingine akatoka katika hekalu, kwa santi kuu akimlilia yeye aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu, Tia mundu wako, ukavune; kwa kuwa saa ya kuvima imekuja; kwa kuwa mavimo ya inchi yamekomaa. 16 Na yeye aliyeketi juu ya wingu akautupa mundu wake juu ya inchi, inchi ikavunwa. 17 Malaika mwingine akatoka katika hekalu iliyo mbinguni, yeye nae ana mundu mkali. 18 Na malaika mwingine akatoka katika ile madhbabu, mwenye mamlaka juu ya moto; kwa sauti kuu akamlilia yule mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume matawi va mzabibu wa inchi, maana zabibu zake zimewiva sana. 19 Malaika yule akautupa mundu wake hatta inchi, akauchuma mzabibu wa inchi, akatupa katika shinikizo la hasira ya Mungu, lile kubwa. 20 Shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, damu ikatoka katika shinikizo mpaka khatamu za farasi, mwendo wa mastadio elfu na sita mia. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania