Ufunuo 13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 NIKASIMAMA juu ya mchanga wa bahari. Nikaona nyama akitoka katika bahari niwenye vichwa saba, na pembe kumi, na juu ya pembe zile vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya ukafiri. 2 Na yule nyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubba, na kinywa chake kama kinywa cha simba; yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi. 3 Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimejeruhi jeraha ya mauti. Pigo lake la mauti likaponywa, dunia yote ikastaajabu nyama ya nyama yule. 4 Wakamsujudu yule joka aliyempa nyama uwezo, wakamsujudu yule nyama, wakisema, Nani afananae na nyama? Nani awezae kufanya vita nae? 5 Akapewa kinywa kunena maneno makuu, ya ukafiri. Akapewa uwezo kufanya kazi yake miezi arubaini na miwili. 6 Akafunna kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni. 7 Akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya killa kabila na lugba na taifa. 8 Watu wote wakaao juu ya inchi wakamsujudu, ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia. 9 Mtu akiwa na sikio na asikie. 10 Mtu akichukua mateka achukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hivyo ndivyo uvumilivu na imani ya watakatifu. 11 Nikaona nyama mwingine akipanda juu kutoka inchi, nae alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana Kondoo, akanena kama joka. 12 Atumia uweza wote wa nyama yule wa kwanza mbele yake, na kuifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie nyama wa kwanza, ambae jeraha yake ya mauti iliponywa. 13 Nae afanya ishara kubwa, hatta afanye moto kushunka kutoka mbinguni juu ya inchi mbele ya wana Adamu. 14 Nae awakosesha wakaao juu ya inchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya nyama, akiwaambia wakaao juu ya inchi kumfanyia sanamu yule nyama aliyekuwa na jeraha ya mauti akaishi. 15 Akapewa kutia pumzi katika sanamu ya nyama, hatta ile sanamu ya nyama inene, na kufanya wo wote wasioisujudu sanamu ya nyama wanawe. 16 Nae awahinya wote, wadogo na wakuu na matajiri na maskini na walio huru na watumwa, watiwe alama katika mkono wao wa kuume au katika vipaji vya nyuso zao: 17 tena kwamba mtu aliye yote asimmne wala kuuza, isipokuwa ana alama ile au jimi la nyama yule, au hesabu ya jina lake. 18 Hapo udipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya nyama huyo: maana ni hesabu ya mwana Adamu; na hesabu yake ni Sita mia, sittini na sita. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania