Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ufunuo 11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 NIKAPEWA mwanzi kama ufito mmoja, akaniambia, Inuka, ukaipime hekalu ya Mungu, na madhbabu, nao wasujuduo humo.

2 Na behewa iliyo nje ya hekalu uitupe nje wala usiipime, kwa maana mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arubaini na miwili.

3 Nami nitawarukhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na miateen na sittini, wamevikwa mavazi ya kigunia.

4 Hawo ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele ya Mungu wa inchi.

5 Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa.

6 Hawa wana mamlaka kuzifunga mbingu, illi mvua isinye katika siku za unabii wao. Na wana mamlaka juu ya maji kuyagenza kuwa damu, na kuipiga inchi kwa killa pigo, killa watakapo.

7 Hatta watakapoumaliza ushuhuda wao yule nyama atokae katika abuso atafanya vifa nao, nae atawashinda na kuwaua.

8 Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wetu aliposulibiwa.

9 Na watu wa hawo jamaa na kabila na lugha na taifa wataitazama mizoga yao siku tatu u nussu, wala hawataiacha mizoga yao kuwekwa kaburini.

10 Nao wakaao juu ya inchi watafanya furaha juu yao ua kushangilia. Na watapelekeana zawadi kwa kuwa manabii hawo wawili waliwatesa wao wakaao juu ya inchi.

11 Na baada ya siku tatu u nussu roho ya uhayi itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama, khofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama.

12 Nikasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, Pandeni hatta huku. Wakapanda mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama.

13 Na katika saa ile palikuwa na tetemeko la inchi, nalo kubwa, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka, wana Adamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na khofu wakamtukuza Mungu wa mbingu.

14 Ole wa pili umekwisha pita, tazama ole wa tatu anakuja upesi.

15 Malaika wa saha akapiga baragumu, pakawa sauti kuu katika mbingu, zikisema, Falme za dunia zimekwisha kuwa ufalme na Mungu na wa Kristo wake, nae atamiliki hatta milele na milele.

16 Na wale wazee ishirini na wane waketio mbele ya Mungu katika viti vya enzi vyao wakaanguka kifudifudi, wakamsujudu Mungu,

17 wakisema, Tunakushukuru, Bwana Mungu Mwenyiezi, ulioko, na nliyekuwako, kwa sababu umetwaa uweza wako ulio mkuu, ukamiliki.

18 Na mataifa walighadhabika, ghadhabu yako ikaja, na wakati wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako manabii na watakatifu, nao walichao jina lako, wadogo na wakubwa, na wa kuwaharibu hawo waiharibuo inchi.

19 Hekalu ya Mungu ikafunguliwa mbinguni na sanduku la agano likaonekana ndani ya hekalu yake. Kukawa umeme, na sauti, na radi, na tetemeko, na mvua ya mawe uyingi sana.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo