Tito 1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 PAOLO, mtumwa wa Mungu, mtume wa Yesu Kristo, illi ienee imani ya wateule wa Mungu, na ujuzi wa kweli iletayo utawa, 2 katika tumaini la nzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema nwongo aliuahidi kabla ya nyakati za zamani; 3 akalifunua neno lake kwa nyakati zake katika ule ujumbe nilioaminiwa mimi kwa amri ya Mwokozi wetu, Mungu: 4 kwa Tito, mwanangu katika imani tuishirikiyo: Neema na rehema na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo, Mwokozi wetu. 5 Kwa sababu hii nalikuaeba katika Krete, illi nyatengeneze yaliyosalia, na kuweka wazee katika killa mji kama nilivyokuamuru; 6 ikiwa mtu hakushitakiwa neno, nae ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni asharati na wasiotii. 7 Maana imempasa askofu awe mtu asioshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa Mungu; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mzoelea mvinyo, asiwe mpigaji, asiwe mpenda mapato ya aibu, 8 bali awe mkaribishaji, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kujimudu nafsi yake; 9 alishikae neno la imani kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupingana nae. 10 Maana wako wengi wasiotii, wenye maneno yasiyo maana, wadanganyaji, khassa wale waliotahiriwa, 11 ambao yapasa wazibwe vinywa vyao. Hawo wanapindua uyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu. 12 Mtu wa kwao, nabii wao wenyewe, amesema. Wakrete ni wawongo siku zote, nyama mwitu wahaya, walafi, wasiofanya kazi. Ushuhuda huu ni kweli. 13 Kwa sababu hiyo uwakemee kwa ukali wapate uzima katika Imani, 14 wasisikilize hadithi za Kiyahudi, na maagizo ya wana Adamn wajiepushao na kweli. 15 Vitu vyote ni sali kwao walio safi: lakini hapana kilicho safi kwa walio najis, wasioamini, bali akili zao na nia zao pia zimekuwa najis. 16 Wanakiri kwamha wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana, ni wenye machukizo, maasi, na kwa killa tendo jema hawafai. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania