Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 AKAPANDA chomboni, akavuka, akafika mjini kwake.

2 Wakamletea mgonjwa wa kupooza, amelala kitandani: na Yesu, akiona imani yao, akamwambia yule mgonjwa wa kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanaugu; umeondolewa dhambi zako.

3 Baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru.

4 Nae Yesu, akijua mawazo yao, akasema, Jinsi gani mnawaza maovu mioyoni mwenu?

5 Kwa maana vipi vyepesi, kusema, Umeondolewa dhambi zako; au kusema, Ondoka, ukaende?

6 Lakini illi mjue ya kuwa Mwana wa Adamu yuna mamlaka katika dunia kuondoa dhambi, (amwambia yule mgonjwa wa kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, ukaende nyumbani kwako.

7 Akaondoka, akaenda zuke nyumbani kwake.

8 Makutano wakimwona, wakastaajabu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu mamlaka ya jinsi hii.

9 Yesu alipokuwa anaondoka kutoka huko akaona mtu amekeli fordhani, aitwae Mattayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata.

10 Ikawa alipoketi ale ndani ya nyumba, wutoza ushuru wengi na wenye dhambi wakaja wakaketi pamoja na Yesu ua wanafunzi wake.

11 Mafarisayo walipoona, wakawaambia wanafunzi wake, Kwa nini mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?

12 Nae Yesu akisikia, akawaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi.

13 Lakini shikeni njia, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka: kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu.

14 Wakati ule wanafunzi wa Yohana wakamwendea, wakinena, Kwa nini sisi na Mafarisayo twafunga marra nyingi, bali wanafunzi wako hawafungi?

15 Yesu akawaambia, Wana wa arusi wawezaje kuomboleza, maadam Bwana arusi yupo pamoja nao? Lakini siku zitakuja atakapoondolewa bwana arusi; udipo watakapofunga.

16 Hakuna mtu atiae kipande cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, likazidi kutatuka.

17 Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; ikiwa watia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, vile viriba vikaharibika: bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote.

18 Alipokuwa akiwaambia haya, yuaja jumbe mmoja, akamsujudia, akinena, Binti yangu udio kwanza afe: lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, uae atapona.

19 Akaondoka Yesu, akamfuata, pamoja na wanafunzi wake.

20 Na mwanamke, aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka thenashara, alikuja kwa nyuma, akagusa upindo wa vazi lake:

21 kwa maana alisema kimoyomoyo, Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona.

22 Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile.

23 Yesu alipofika nyumbani kwa yule jumbe, akaona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo,

24 akawaambia, Ondokeni: kwa maana kijana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana.

25 Hatta makutano walipoondoshwa, akaingia, akamshika mkono wake; yule kijana akasimama.

26 Zikaenea khabari hizi katika inchi ile yote.

27 Yesu alipokuwa anaondoka kutoka huko, vipofu wawili wakamfuata wakipaaza sauti, wakinena. Uturehemu, Ee mwana wa Daud.

28 Alipolika nyumbani, wale vipofu wakamwendea: Yesu akawaambia. Mnaamini kwamba naweza kufanya haya? Wakamwambia, Naam, Bwana.

29 Marra akawagusa macho yao, akanena, Kwa kadiri ya imani yenu mpate.

30 Macho yao yakafumbuka. Yesu akawaagiza kwa nguvu, akinena, Angalieni hatta mtu mmoja asijue.

31 Lakini wakatoka, wakaeneza khabari zake katika inchi ile yote.

32 Hatta wale walipokuwa wakitoka, wakamletea mtu bubu mwenye pepo.

33 Na pepo alipofukuzwa, yule bubu akasema, makutano wakastaajabu, wakanena, Haijaonekana hivi katika Israeli wakati wo wote.

34 Lakini Mafarisayo wakanena, Kwa mkuu wa pepo afukuza pepo.

35 Na Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masunagogi yao, akikhubiri injili ya ufalme, akiponya magonjwa yote na dhaifu zote katika watu.

36 Na alipowaona makutano, akawahurumia, kwa maana walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchunga.

37 Ndipo akawaambia wanafunzi wake, Mavuno ni makubwa, bali watenda kazi wachache.

38 Bassi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo