Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 ALIPOSHUKA mlimani, makutano mengi walimfuata.

2 Akaja mwenye ukoma akamsujudu, akinena, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa.

3 Yesu akanyosha mkono wake, akamgusa, akinena, Nataka: takasika. Marra ukoma wake ukatakasika.

4 Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; illa enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, utoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.

5 Hatta Yesu alipoingia Kapernaum, akida alimjia, akamsihi,

6 akinena, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana.

7 Yesu akamwambia. Nitakuja, nimponye.

8 Akida akamjibu, akasema, Si stahili yangu wewe uingie chini ya dari yangu: lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.

9 Maana na mimi ni mtu chini ya mamlaka, nina askari chini yangu: nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; au mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.

10 Yesu aliposikia haya, akastaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa kama hii, hatta katika Israeli.

11 Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magbaribi, wataketi pamoja na Ibrabimu, na Isaak, na Yakob katika ufalme wa mbinguni;

12 bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje; ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno.

13 Yesu akamwambia akida, Nenda zako: na kadiri ulivyoamini upate. Mtumishi wake akapona saa ileile.

14 Hatta Yesu alijiofika nyumbani kwa Petro, akamwona mama wa mkewe amelala hawezi homa.

15 Akamgusa mkono wake, homa ikamwacha; nae akaondoka, akawatumikia.

16 Ilipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo: akawafukuza pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi,

17 illi litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe alitwaa magonjwa yetu, na kuchukua maradhi zetu.

18 Yesu alipoona makutano mengi wakimzunguka, akaamuru kuvuka hatta ngʼambu.

19 Mwandishi mmoja akamwendea, akamwambia, Mwalimu, nitakufuata ko kote uendako.

20 Yesu akamwambia, Mbweha wana matundu, na ndege za anga vituo; bali Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake.

21 Mwingine katika wanafunzi wake akamwambia, Bwana, nipe rukhusa kwanza, niende nikamzike baba yangu.

22 Lakini Yesu akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao.

23 Akapanda chomboni, wanafunzi wake wakamfuata.

24 Kukawa msukosuko mkuu baharini, hatta chombo kikafunikizwa na mawimbi: nae alikuwa amelala.

25 Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha, wakinena, Bwana, tuokoe tunaangamia.

26 Akawaambia, Mbona mu waoga, enyi wa imani haba? Marra akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu.

27 Wale watu wakastaajabu, wakinena. Huyo ni mtu wa namna gani hatta pepo na bahari zamtii?

28 Alipofika ngʼambu, katika inchi ya Wagergesene, watu wawili wenye pepo walikutana nae, wanatoka makaburini, wakali mno, hatta mtu asiweze kupita njia ile.

29 Wakapiga kelele, wakinena, Tuna nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu? Je, umekuja kutuadhibu kabla ya muhulla?

30 Bassi, kulikuwako mbali kundi la nguruwe wengi wakilisha.

31 Pepo wakamsihi, wakinena, Ukitufukuza, tuache twende, tukaingie katika kundi la nguruwe.

32 Akawaambia. Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika kundi la nguruwe: na, kumbe! kundi lote la nguruwe likatelemka kwa kassi gengeni, wakaingia baharini, wakafa majini.

33 Wachungaji wakakimbia, wakaenda zao mjini, wakayakhubiri yote, na mambo ya wenye pepo pia.

34 Mji wote ukatoka kwenda kumlaki Yesu; walipomwona, wakamsihi aondoke mipakani mwao.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo