Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 MSIHUKUMU, illi msihukumiwe

2 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa: na kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa.

3 Nawe, ya nini kukitazama kibanzi kilicho katika jicho la ndugu yako, na boriti iliyo katika jicho lako huiangalii?

4 Au utamwambiaje ndugu yako, Niache niondoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! imo boriti ndani ya jicho lako?

5 Mnaflki, iondoe kwanza ile boriti katika jicho lako; ndipo utakapoona sana hatta kukiondoa kibanzi katika jicho la ndugu yako.

6 Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararueni.

7 Ombeni na mtapewa; tafuteni na mtaona; bisheni na mtafunguliwa:

8 kwa maaua killa aombae hupokea; nae atafutae huona, nae abishae alafunguliwa.

9 Au mtu yupi katika ninyi, ambae, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe?

10 Au akiomba samaki, atampa nyoka?

11 Kama ninyi, bassi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! si zaidi Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wamwombao?

12 Bassi yo yote mtakayo kutendewa na watu, nanyi mwatendee vivyo hivyo: maana hiyo ndiyo torati na manabii.

13 Ingieni kwa kupita mlango ulio mwembamba: maana ujia iendayo hatta upotevu ni pana, na mlango wake mpana, na wengi waingiao kwa mlango huo.

14 Bali njia ni nyembamba iendayo hatta uzima, na mlango wake ni mwembamba: nao waionao ni wachache.

15 Jihadharini na manabii wa uwongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa wa mwitu wakali.

16 Mtawalambua kwa matunda yao. Je, watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?

17 Vivyo hivyo killa mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti uliopea huzaa matunda hafifu.

18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda hafifu, wala mti uliopea kuzaa matunda mazuri.

19 Killa mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.

20 Bassi kwa matunda yao mtawatambua.

21 Siye killa mtu aniambiae, Bwana, Bwana, atakaeingia katika ufalme wa mbinguni; hali yeye afanyae mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kufukuza pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwafahamu ninyi wakati wo wote: ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

24 Bassi killa asikiae haya maneno yangu, na kuyafanya, nitamfananisha na mtu mwenye akili aliyejenga nyumba vake juu ya mwamba:

25 mvua ikanya, maji mengi yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa katika mwamba.

26 Na killa asikiae haya maneno yangu, asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, alivejenga nyumba yake katika mchanga;

27 mvua ikanya, maji mengi yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; anguko lake likawa kubwa.

28 Ikawa, Yesu alipomaliza maneno haya, makutano wakashangaa kwa mafundisho yake:

29 kwa maana alikuwa akiwafundisha kwa namna ya mwenye mamlaka, wala si kama waandishi wao.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo