Mathayo 6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 ANGALIENI msitoe sadaka zenu mbele ya watu, kusudi mtazamwe nao: kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. 2 Bassi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika sunagogi na njiani, illi watukuzwe na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. 3 Bali wewe utoapo sadaka, hatta mkono wako wa kushoto usijue mkono wako wa kuume ufanyalo; 4 sadaka yako iwe kwa siri: na Baba yako aonae kwa siri atakujazi kwa dhahiri. 5 Tena usalipo, usiwe kama wanafiki: kwa maana wapenda kusali wakisimama katika sunagogi na katika pembe za njia, illi waonekane na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. 6 Bali wewe usalipo, ingia chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele ya Baba yako aliye kwa siri: na Baba yako aonae kwa siri atakujazi kwa dhahiri. 7 Mkiwa katika kusali, msipayukepayuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. 8 Bassi msifanane na hawo; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. 9 Bassi ninyi salini hivi; Baba yetu nliye mbinguni, jina lako takatifu litukuzwe, 10 Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. 11 Utupe leo riziki zetu. 12 Utusamehe deni zetu, kama sisi tunavyowasamehe wadeni wetu. 13 Usitutie majaribuni, bali utuokoe na yule mwovu. 14 Kwa kuwa wako ni ufalme, na nguvu, na utukufu, hatta milele. Amin. Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe nanyi. 15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. 16 Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana: maana hujiumbua nyuso zao, illi waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambieni, wamekwisha kupata thawabu yao. 17 Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe nso; 18 illi usionekane na watu kuwa unafunga, bali na Baba yako aliye kwa siri; na Baba yako, aonae kwa siri, atakujazi kwa dhahiri. 19 Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu ziharibupo, na wevi huvunja na kuiba: 20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, zisikobaribu nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala kuiba; 21 kwa maana ilipo hazina yenu, ndipo utakapokuwa na moyo wako. 22 Taa ya mwili ni jicho; bassi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru. 23 Lakini jicho lako likiwa ovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Bassi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza, giza gani hilo! 24 Hakuna mtu awezae kuwatumikia bwana wawili; kwa maana atamchukia mmoja, na kumpenda wa pili; au atamshika mmoja, na kumtweza wa pili. Hamwezi kumtumikia Mungu na mamona. 25 Kiva sababu hii nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mleni au mnyweni; wala mwili wenu, mvaeni. Maisha je, si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? 26 Waangalieni ndege wa anga, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni awalisha hawo. Ninyi je! si bora kupita hawo? 27 Yupi katika ninyi awezae kwa kusumbuka kujiongeza kimo chake mkono mmoja? 28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini khabari za maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayatendi kazi, wala hayasokoti: 29 lakini nawaambieni, ya kwamba hatta Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama moja la hayo. 30 Lakini Mungu akiyavika hivi majani ya mashamba, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je, hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? 31 Msisumbuke, bassi, mkinena, Tuleni? au, Tunyweni? au, Tuvaeni? 32 Kwa maana haya yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji haya yote. 33 Bali utafuteni kwanza ufalme wa Mungu, na haki yake; na haya yote mtazidishiwa. 34 Bassi msisumbukie kesho; kwa kuwa kesho itayasumbukia mambo yake. Watosba kwa siku ubaya wake. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania