Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 NAE akivaona makutano, akapanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake wakamjia;

2 akafunua kinywa chake, akawafundisha, akinena,

3 Wa kheri walio maskini wa roho; maana ufalme wa mbinguni ni wao.

4 Wa kheri wenye huzuni: maana hawo watafarajika.

5 Wa kheri wenye upole: maana hawo watairithi inchi.

6 Wa kheri wenye njaa na kiu ya haki: maana hawo watashiba.

7 Wa kheri wenye rehema: maana hawo watarehemiwa.

8 Wa kheri walio na moyo safi; maana hawo watamwona Mungu.

9 Wa kheri wasuluhishi: maana hawo watakwitwa wana wa Mungu.

10 Wa kheri wateswao kwa ajili ya haki: maana ufalme wa mbinguni ni wao.

11 M kheri ninyi watakapowatukana na kuwatesa na kuwanenea killa neno baya kwa uwongo, kwa ajili yangu.

12 Furahini, shangilieni: kwakuwa thawabu yenu nyingi mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowatesa manabii waliokuwa kabla yenu.

13 Ninyi ni chumvi ya dunia: lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwani ikolee? Haifai tena kabisa, illa kufupwa nje na kukanyagwa na watu.

14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kustirika ukiwa juu ya mlima.

15 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya kibaba, bali juu ya kibao cha kuwekea taa; nayo yaangaza wote waliomo nyumbani.

16 Vivi hivi nuru yenu iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wakamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

17 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.

18 Kwa maana, amin nawaambieni, Mpaka mbingu na inchi zitakapoondoka, yodi moja na nukta moja ya torati haitaondoka, mpaka yote yatimie.

19 Bassi mtu atakaevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha wafu hivi, atakwitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni: bali mtu atakaezitenda na kufundisha, huyu afakwitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.

20 Maana nawaambieni, Haki yenu isipozidi kuliko haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

21 Mmesikia watu wa kale walivyoanibiwa, Usiue; na mtu akiua, itampasa hukumu.

22 Bali mimi nawaambiem, Killa amwoneae ndugu yake ghadhabu bila sababu, itampasa hukumu; na mtu akimwambia ndugu yake, Haka, itampasa baraza; na mtu akinena, Mpumbavu, itampasa jebannum ya moto.

23 Bassi ukileta sadaka yako madhbahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,

24 iache sadaka yako mbele ya madbbahu, nenda zako, kwanza patana na ndugu yako, kisha rudi utoe sadaka yako,

25 Patana na mshtaki wako upesi, wakati uwapo pamoja nae njiani; yule mshtaki asije akakupeleka kwa kadhi, kadhi akakutia mkononi mwa askari, ukatupwa kifungoni.

26 Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hatta uishe kulipa pesa ya mwisho.

27 Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usizini:

28 Bali mimi miwaambieni, Killa mtu atazamae mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini nae moyoni mwake.

29 Jicho lako la kuume likikukosesha, lingʼoe ulitupe mbali nawe: kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehannum.

30 Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe: kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee, wala mwili wako mzima usitupwe katika jehannum.

31 Waliambiwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe khati ya talaka;

32 bali mimi nawaambieni, Killa mtu amwachae mkewe, isipokuwa kwa khabari ya asharati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.

33 Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usifanye zuli, bali mtimizie Bwana nyapo zako;

34 bali mimi nawaambieni, Usiape kabisa; hatta kwa mbingu, kwa maana ndio kiti cha enzi cha Mungu;

35 wala kwa inchi, kwa maana ndio pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemi, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.

36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unyele mmoja kuwa mwenpe au mwensi.

37 Bali maneno yenu yawe, Ndio, ndio; Sio, sio: kwa kuwa izidiyo haya yatoka kwa yule mwovu.

38 Mmesikia walivyoambiwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino:

39 bali mimi nawaambieni, Msishindane na mtu mwovu; bali mtu akupigae shavu la kuume, mgeuzie na la pili.

40 Na mtu atakae kukushtaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho.

41 Na mtu atakaekutumikisha maili moja, nenda nae mbili.

42 Akuombae, mpe; nae atakae kukopa kwako, usimpe kisogo.

43 Mmesikia walivyoambiwa, Mpende jirani yako, na, Mchukie adui yako:

44 bali mimi nawaambieni, Wapendeni adui zenu, wabarikini wanaowalaani, watendeni mema wanaowachukia, waombeeni wanaowatendea ukorofi, na kuwatesa;

45 illi mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni: maana yeye jua lake huwazushia waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.

46 Maana mkiwapenda wanaowapendani, mwapata thawabu gani? Hatta watoza ushuru, je, nao hawafanyi yayo hayo?

47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziyada? Hatta wattoza ushuru, je, nao hawafanyi kama hayo?

48 Bassi mwe ninyi wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo