Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 NDIPO Yesu alipopandishwa na Roho hatta jangwani, illi ajaribiwe na Shetani.

2 Akafunga siku arubaini mchana na usiku, baadae akaona njaa.

3 Mjaribu akamjia akasema, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.

4 Akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, illa kwa killa neno litokalo katika kinywa cha Mungu.

5 Kisha Shetani akamchukua hatta mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu, akamwambia,

6 Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini: kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake: Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

7 Yesu akamwambia. Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.

8 Tena Shetani akamchukua hatta mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fakhari yake, akamwambia,

9 Hizi zote nitakupa, ukianguka kunisujudia.

10 Ndipo Yesu akamwambia, Nenda zako, Shetani: kwa maana imeandikwa, Utamsujudia Bwana Mungu wako, nae peke yake utamwabudu.

11 Kisha Shetani akamwacha; wakaja malaika wakamtumikia.

12 Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, akaenda zake hatta Galilaya;

13 akatoka Nazareti, akaenda, akakaa Kapernaum, ulioko pwani, mipakani mwa Zabulon na Nafthalim:

14 illi litimie neno lililonenwa na Nabii Isaya, akisema,

15 Inchi ya Zabulon na inchi ya Nafthalim, Njia ya bahari ngʼambu ya Yordani, Galilaya ya mataifa,

16 Watu waliokaa gizani Waliona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika inchi na kivuli cha mauti, Mwanga umewazukia.

17 Tokea wakati huo Yesu akaanza kukhubiri, na kusema, Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia.

18 Nae Yesu akitembea kando ya bahari ya Galilaya, akaona ndugu wawili, Simon aitwae Petro, na Andrea ndugu yake, wakitupa jarife baharini; maana walikuwa wavuvi.

19 Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wii watu.

20 Marra wakaziacha nyavu, wakamfuata.

21 Akaendelea mbele, akaona ndugu wengine wawili. Yakob wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake, walikuwa katika chombo pamoja na Zebedayo baba yao, wakitengeneza nyavu zao; akawaita.

22 Marra wakakiacha chombo na baba yao, wakamfuata.

23 Yesu akazunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika sunagogi zao, na kuikhubiri injili ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa killi namna katika watu.

24 Khabari zake zikaenea katika Sham yote; wakamletea watu waliokuwa hawawezi, walioshikwa mi maradhi mbali mbali na mateso, nao wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.

25 Makutano mengi wakamfuata, wakitoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemi, na Yahudi, na ngʼambu ya Yordani.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo