Mathayo 3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 SIKU zile akaondokea Yohana Mbatizaji akikhubiri katika jangwa ya Yahudi, akinena, 2 Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. 3 Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti yake apigae mbin jangwani, Itengenezeni njia ya Bwana, Nyosheni mapito yake. 4 Yohana mwenyewe alikuwa na mavazi yake ya singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu. 5 Ndipo wakamwendea Yerusalemi, na Yahudi yote, na inchi zote za kando za Yordani; 6 wakabatizwa nae mtoni Yordani, wakiziungama dhambi zao. 7 Hatta akiona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, akawaambia, Uzao wa nyoka, nani aliyewaonya mkimbie ghadhabu ijayo? 8 Zaeni bassi matunda yaipasayo toba; 9 msiwaze moyoni kwamba, Tuna baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambieni ya kwamba Mungu anaweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto. 10 Nalo shoka limekwisha kuwekwa penye shina la miti; bassi killa mti usiozaa matunda mazuri unakatwa na kutupwa motoni. 11 Mimi nawabatizeni katika maji mpate kutubu: bali yeye ajae nyuma yangu ni hodari kuliko mimi, wala sistahili hatta kuchukua viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 12 Pepeto lake li mkononi mwake, nae ataitakasa sana sakafu yake; atakusanya nganu yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika. 13 Ndipo Yesu akafika hatta Yordani kwa Yohana kutoka Galilaya illi abatizwe nae. 14 Lakini Yohana alikuwa akimzuia, akinena, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, na wewe waja kwangu? 15 Yesu akajibu, akamwambia, Hayo yaache sasa: kwa kuwa hivi imetupasa kutimiza haki yote. Bassi akamwacha. 16 Nae Yesu alipokwisha kubatizwa marra akapanda kutoka majini: mbingu zikamfunukia, akamwona Roho ya Mungu akishuka kama hua, akija juu yake: 17 na sauti toka mbinguni ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninaependezwa nae. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania