Mathayo 28 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 SABATO ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, akaenda Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, kulitazama kaburi. 2 Na kumbe! palikuwa na tetemeko kubwa la inchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka mbinguni, akakaribia akalifingirisha lile jiwe mbali ya mlango, akaketi juu yake. 3 Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama thuluji. 4 Na kwa kumwogopa walinzi wakatetemeka, wakawa kama wafu. 5 Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnanitafuta Yesu aliyesulibiwa. 6 Hayupo hapa; kwa maana amefufuka kama alivyosema. Njoni, patazameni mahali alipolazwa Bwana. 7 Shikeni njia upesi, kawaambieni wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu; Tazama, anatangulia mbele yenu kwenda Galilaya; huko mtamwona: haya, nimewaambieni. 8 Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa khofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake khabari. 9 Nao walipokuwa wakienda kuwapasha wanafunzi wake khabari, Yesu akakutana nao, akinena, Salam! Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia. 10 Yesu akawaambia, Msiogope: enendeni, mkawaambie ndugu zangu waemle Galilaya, ndiko watakakoniona. 11 Nao walipokuwa wakienda njiani, baadhi ya askari waliingia mjini, wakawapasha makuhani wakuu khabari za mambo yote yaliyotendeka. 12 Wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi, 13 wakinena, Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala. 14 Na jambo hili likisikilikana kwa liwali, tutasema nae, nanyi tutawaondoa shaka. 15 Bassi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno lile likaenea katika Wayahudi hatta leo. 16 Na wale wanafunzi edashara wakaenda Galilaya hatta mlima ule aliowaagiza Yesu. 17 Nao walipomwona, wakamsujudia; lakini wengine waliona shaka. 18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akinena, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na juu ya dunia. 19 Bassi, enendeni, kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20 mkiwafundisha kushika yote niliyowaamuru ninyi: nti tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hatta mwisho wa dunia. Amin. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania