Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 27 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 ILIPOKUWA assubuhi, makuhani wakuu wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumfisha;

2 wakamfunga, wakamchukua, wakampeleka kwa liwali Pontio Pilato.

3 Ndipo Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, akajuta, akawarudishia makuhani wakuu na wazee vile vipande thelathini vya fedha,

4 akinena, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na khatiya. Wakanena, Bassi, haya yatukhussu nini sisi? Tazama wewe hayo.

5 Akavitupa vile vipande vya fedha katika patakatifu, akaondoka; akaenda, akajinyonga.

6 Makuhani wakuu wakavitwaa vile vipande vya fedha, wakasema, Ni haramu kuviweka katika sanduku ya sadaka, kwa kuwa ni kima cha damu.

7 Wakafanya shauri, wakavitumia kwa kununua konde la mfinyangi liwe mahali pa kuzikia wageni.

8 Kwa hiyo konde lile linakwitwa konde la damu, hatta leo.

9 Ndipo likatimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema, Wakavitwaa vipande thelathini vya fedha, kima chake aliyetiwa kima, ambae watu miongoni mwa wana wa Israeli walimtia kima;

10 wakavitumia kwa kununua konde la mfinyangi, kama Bwana alivyoniagiza.

11 Yesu akasimama mbele ya liwali: liwali akamwuliza, akinena, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Yesu akamwambia, Wewe wanena.

12 Aliposhitakiwa na makuhani wakuu na wazee, hakujibu hatta neno.

13 Ndipo Pilato akamwambia, Husikii mambo mangapi wanayokushuhudia?

14 Nae hakumjibu hatta kwa neno moja, hatta liwali akataajabu sana.

15 Bassi wakati wa siku kuu liwali desturi yake huwafungulia makutano mfungwa mmoja waliyemtaka.

16 Bassi walikuwa na mfungwa mashuhuri siku zile, jina lake Barabba.

17 Bassi walipokutanika, Pilato akawaambia, Mnataka niwafungulie nani? Barabba, au Yesu aitwae Kristo?

18 Kwa maana alijua ya kuwa wamemtoa kwa husuda.

19 Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki: kwa sababu nimeteswa mengi leo katika udoto kwa ajili yake.

20 Nao makuhani wakuu na wazee wakawashawishi makutano illi wamtake Barabba, na kumwangamiza Yesu.

21 Lakini liwali akajibu, akawaambia, Mnataka niwafungulie nani katika hawo wawili? Wakasema, Barabba.

22 Pilato akawaambia, Bassi, nimtendeni Yesu aitwae Kristo? Wakanena wote, Asulibiwe.

23 Liwali akasema, Kwani? ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, wakinena, Asulibiwe.

24 Pilato alipoona ya kuwa hafai neno, bali ya kuwa inazidi kuwa ghasia, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya makutano, akasema, Mimi sina khatiya kwa khabari ya damu ya mtu huyu mwenye haki: tazameni hayo ninyi wenyewe.

25 Watu wote wakajibu wakasema, Damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu.

26 Ndipo akawafungulia Barabba: na alipokwisha kumpiga Yesu mijeledi, akamtoa apate kusulibiwa.

27 Ndipo askari wa liwali wakamchukua Yesu ndani ya praitorio, wakamkusanyia kikosi kizima.

28 Wakamvua nguo, wakamvika vazi jekundu.

29 Wakasokota taji ya miiba, wakaiweka juu ya kichwa chake, na unyasi katika mkono wake wa kuume; wakapiga magoti mbele yake, wakamfanyizia dhihaka, wakinena, Salamu, Mfalme wa Wayahudi!

30 Wakamtemea mate, wakautwaa ule unyasi, wakampiga kichwa.

31 Walipokwisha kumfanyia dhihaka, wakalivua lile vazi, wakamvika nguo zake, wakamchukua kumsulibi.

32 Hatta walipokuwa wakitoka humo, wakakutana na mtu Mkurene, jina lake Simon; huyu wakamtumikisha auchukue msalaba wake.

33 Walipofika mahali paitwapo Golgotha, maana yake, Mahali pa kichwa,

34 wakampa kunywa siki iliyochanganyika na safura; nae alipoonja hakutaka kunywa.

35 Walipokwisha kumsulibi, wakagawa nguo zake, wakipiga kura: illi litimie neno lililonenwa na nabii. Waligawa nguo zangu kati yao, na juu ya vazi langu walipiga kura.

36 Wakaketi, wakamwangalia huko.

37 Wakaweka juu ya kichwa chake mshitaka wake, ulioandikwa, HUYU NI YESU, MFALME WA WAYAHUDI.

38 Ndipo wanyangʼanyi wawili wakasulibiwa pamoja nae, mmoja mkono wake wa kuume, na mmoja mkono wake wa kushoto.

39 Nao waliokuwa wakipita njiani wakamtukana, wakitikisatikisa vichwa vyao,

40 wakinena, Ewe ulivunjae hekalu na kuijenga kwa siku tatu, jiponye nafsi yako; ukiwa Mwana wa Mungu, shuka msalahani.

41 Kadhalika ua wale makuhani wakuu wakimdhihaki pamoja na waandishi na wazee, wakinena,

42 Aliponya watu wengine, hawezi kujiponya nafsi yake. Akiwa mfalme wa Israeli, na ashuke sasa msalabani, naswi tutamwamini.

43 Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kamii akimtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu.

44 Vilevile wa ayangʼanyi nao waliosulibiwa pamoja nae walimshutumu.

45 Tangu saa sita palikuwa giza juu ya inchi yote hatta saa tissa.

46 Na kama saa tissa, Yesu akapaaza sauti yake kwa nguvu akinena, Eli, Eli, lama sabakhthani? maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?

47 Baadhi yao waliosimama huko, waliposikia, wakanena, Huyu anamwita Elia.

48 Marra mmoja wao akaenda mbio, akatwaa sifongo, akaijaza siki, akaitia juu ya unyasi, akamnywesha.

49 Wale wengine walinena, Acha; na tuone kwamba Elia anakuja kumponya.

50 Nae Yesu akiisha kupaaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.

51 Na tazama pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hatta chini: inchi ikatetema; miamba ikapasuka;

52 makaburi yakafunuka; ikafufuka miili mingi ya watakatifu waliolala;

53 nao wakiisha kutoka makaburini, baada ya kufufuka kwake, wakaingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.

54 Bassi yule akida, nao walio pamoja nae wakimwangalia Yesu, walipoliona tetemeko la inchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakinena, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.

55 Na palikuwa na wanawake wengi huko wakitazama kwa mbali, hawo ndio waliomfuata Yesu toka Galilaya, na kumtumikia.

56 Miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo na Yose, na mama yao wana wa Zebedayo.

57 Ilipokuwa jioni akafika mtu tajiri wa Arimathaya, jina lake Yusuf, nae mwenyewe alikuwa mwanafunzi wa Yesu;

58 mtu huyu alimwendea Pilato, akauomba mwili wa Yesu. Pilato akaamuru apewe mwili wake.

59 Yusuf akautwaa mwili, akauzinga katika kitambaa cha kitani safi,

60 akanweka katika kaburi lake jipya, alilolikata mwambani; akafingirisha jiwe kubwa hatta mlango wa kaburi, akaenda zake.

61 Walikuwako hapo Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, wameketi kulielekea kaburi.

62 Hatta siku ya pili, ndiyo iliyo baada ya Maandalio, makuhani wakuu na Mafarisayo wakamkusanyikia Pilato,

63 wakinena, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa hayi bado, Baada ya siku tatu nitafufuka.

64 Bassi amuru kaburi lilindwe sana hatta siku ya tatu; wasije wanafunzi wake usiku wakamwiba, wakawaambia watu, Amefufuka katika wafu: na kosa la mwisho litapita lile la kwanza.

65 Pilato akawaambia, Mna askari: enendeni kalilindeni sana kadiri mjuavyo.

66 Wakenda zao, wakalilinda sana kaburi, wakilitia lile jiwe muhuri, pamoja na wale askari walinzi.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo