Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 26 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 IKAWA Yesu alipomaliza maneno haya yote, akawaambia wanafunzi wake,

2 Mwajua ya kuwa baada ya siku mbili itakuwa pasaka, na Mwana wa Adamu atasalitiwa apate kusulibiwa.

3 Ndipo makubani wakuu, na waandishi, na wazee wa watu wakakusanyika katika behewa ya kuhani mkuu aliyeitwa Kayafa;

4 wakafanya shauri pamoja, illi wamkamate Yesu kwa hila na kumwua.

5 Wakanena, Sio wakati wa siku kuu, isije ikatokea ghasia katika watu.

6 Nae Yesu, alipokuwa Bethania katika nyumba ya Simon mwenye ukoma,

7 mwanamke mwenye chombo cha alabastro cha marhamu ya thamani kubwa alimkaribia, akaimimina kichwani pake alipoketi akila.

8 Wanafunzi wake walipoona, wakachukiwa, wakinena, Ya nini upotevu huu?

9 Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa fedha nyingi wakapewa maskini.

10 Yesu akijua akawaambia, Mbona mnamtaabisha mwanamke? Maana ni kazi njema aliyonitendea mimi.

11 Kwa maana siku zote maskini mnao pamoja nanyi; lakini mimi hamnami siku zote.

12 Maana kwa kunimwagia mwili wangu marhamu hii, ametenda hivi illi kuniweka tayari kwa maziko yangu.

13 Amin, nawaambieni, Killa ikhuhiriwapo injili hii katika ulimwengu wote, na hilo alilolitenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake.

14 Kisha mmoja wa wale thenashara, jina lake Yuda Iskariote, alikwenda zake kwa makuhani wakuu,

15 akasema, Nini mtakayonipa, nami nitamsaliti kwenu? Wakampimia vijiande thelathini vya fedha.

16 Tokea wakati huo akawa akitafuta nafasi ajiate kumsaliti.

17 Hatta siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi wake wakamwendea Yesu, wakamwambia, Wapi unataka tukuandalie uile pasaka?

18 Akasema, Enendeni mjini kwa mtu fulani, mkamwambie, Mwalimu anena, Majira yaugu i karibu; kwako nitafanya pasaka pamoja na wanafunzi wangu.

19 Wanafunzi wakatenda kama Yesu alivyowaagiza, wakaiandaa pasaka.

20 Bassi ilipokuwa jioni akaketi chakulani pamoja na wale thenashara.

21 Walipokuwa wakila, akasema, Amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti.

22 Wakahuzunika sana, wakaanza kumwambia mmoja mmoja, Ni mimi, Bwana?

23 Akajibu, akasema, Yeye aliyetia mkono wake pamoja nami katika sahani, ndiye atakaenisaliti.

24 Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa: lakini ole wake mtu yule ambae Mwana wa Adamu anasalitiwa nae! Ingekuwa kheri kwake mtu yule kama asingalizaliwa.

25 Yuda, yule mwenye kumsaliti, akajibu, akasema, Ni mimi, Rabbi? Akamwambia, Wewe umesema.

26 Walipokuwa wakila, Yesu akatwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; huu ni mwili wangu.

27 Akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akinena, Nyweeni nyote hiki;

28 maana hii ni damu yangu ya agano jipya, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.

29 Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu leo nzao huu wa mzabibu, hatta siku ile nitakapounywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.

30 Walipokwisha kuimba, wakatoka nje kwenda mlima wa Mizeituni.

31 Yesu akawaambia, Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili yangu usiku huu: kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchunga, na kondoo wa kundi watatawanyika.

32 Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitatangulia mbele yenu kwenda Galilaya.

33 Petro akajibu, akamwambia, Wajapochukizwa wote kwa ajili yako, mimi sitachukizwa kabisa.

34 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, usiku huu kabla ya kuwika jogoo, utanikana marra tatu.

35 Petro akamwambia, Ijaponipasa kufa nawe, sitakukana. Na wanafuuzi wote wakasema vivi hivi.

36 Kiisha Yesu akaenda pamoja nao hatta kiwanja kiitwacho Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, Ketini hapa, hatta niende kule nikasali.

37 Akamchukua Petro na wana wawili wa Zebedayo, akaanza kufadhaika, na kuhuzunika moyo.

38 Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkakeshe pamoja nami.

39 Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akiomba, akinena, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kinipitie; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.

40 Kisha akawaendea wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! hamkuweza kukesha pamoja nami hatta saa moja?

41 Kesheni, kaombeni, msije mkaingia majaribuni: Roho ina nia njema, bali mwili ni dhaifu.

42 Akaenda tena marra ya pili, akaomba, akinena, Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kinipitie nisipokinywa, bassi, mapenzi yako yafanyike.

43 Akaenda, akawakuta wamelala tena; maana macho yao yalikuwa mazito.

44 Akawaacha tena, akaenda akaomba marra ya tatu, akisema maneno yaleyale.

45 Khalafu akawaendea wanafunzi wake, akawaambia, Laleni sasa hatta mwisho, kapumzikeni: saa imekaribia, na Mwana wa Adamu anatiwa katika mikono ya wenye dbambi.

46 Ondokeni, twende zetu. Angalieni, anaenisaliti anakaribia.

47 Hatta alipokuwa akisema, Yuda, mmoja wa wale thenashara akaja, na pamoja nae makutano mengi, wana panga na marungu, wametoka kwa makuhani wakuu na wazee wa watu.

48 Na yeye anaemsaliti amewapa ishara, akinena, Nitakaembusu, ndiye; mkamateni.

49 Marra akamwendea Yesu, akasema, Salam, Rabbi, akambusu sana.

50 Yesu akamwambia, Rafiki, umejia nini? Wakaenda, wakanyosha mikono yao wakamkamata Yesu.

51 Mmoja wao waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio.

52 Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake: maana wote washikao upanga, wataangamia kwa upanga.

53 Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu sasa hivi, akaniletea zaidi ya majeshi thenashara ya malaika?

54 Yatatimizwaje bassi maandiko, kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kuwa?

55 Saa ile Yesu akawaambia makutano, Je, mmetoka, mfano wa watu wafukuzao mnyangʼanyi mna panga na marungu, kunitwaa? Killa siku naliketi mbele zenu hekaluni, nikifundisha, wala hamkunikamata.

56 Lakini jambo hili lote limekuwa, illi maandiko ya manabii yatimizwe. Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha, wakakimbia.

57 Nao waliomkamata Yesu wakampeleka kwa Kayafa kuhani mkuu, walipokuwapo waandishi na wazee wamekusanyika.

58 Na Petro akamfuata kwa mbali hatta behewa ya kuhani mkuu, akaingia ndani, akaketi pamoja na watumishi, auone mwisho.

59 Makuhani wakuu na baraza yote wakatafuta ushuhuda wa nwongo juu ya Yesu, wapate kumwua;

60 wasipate; na ijapokuwa walitokea mashahidi wa uwongo wengi, hawakupata.

61 Baadae mashahidi wa uwongo wawili wakatokea wakasema, Huyu alisema, Naweza kulivunja hekalu ya Mungu, na kuijenga kwa siku tatu.

62 Kuhani mkuu akasimama akamwambia, Hujibu neno? Hawa wanakushuhudiani?

63 Lakini Yesu akanyamaza. Kuhani mkuu akamjihu, akamwambia, Nakuapisha Mungu aliye hayi, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu.

64 Yesu akamwambia. Wewe umesema: lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwoua Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu.

65 Marra kuhani mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru: tuna haja gani ya mashahidi wengine? Sasa mmesikia kufuru yake:

66 mwaonaje? Wakajibu, wakasema, Ana sharti ya kufa.

67 Ndipo wakamtemea mate va uso, wakampiga konde; wengine wakampiga makofi,

68 wakinena, Ee Kristo, ni nani aliyekupiga?

69 Na Petro alikuwa ameketi nje behewani: kijakazi kimoja akamwendea, akanena, Wewe nawe ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya.

70 Akakana mbele ya wote, akinena, Sijui unenalo.

71 Alipotoka nje hatta ukumbini, mwanamke mwingine akamwona, akawaambia watu waliokuwa huko, Na huyu nae alikuwa pamoja na Yesu Mnazareti.

72 Akakana tena kwa kiapo, Simjui mtu huyu.

73 Punde kidogo, wale waliosimama karibu wakamwendea, wakamwambia Petro, Hakika na wewe u mmoja wao; maana hatta usemi wako wakutambulisha.

74 Ndipo akaanza kulaani na kuapa, Simjui mtu huyu. Marra akawika jogoo.

75 Petro akalikumbuka lile neno la Yesu aliloambiwa nae, Kabla ya kuwika jogoo, utanikana marra tatu. Akatoka nje, akalia kwa majonzi.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo