Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 25 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 NDIPO ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi.

2 Watano wao walikuwa wenye busara, ua watauo wapumbavu.

3 Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao:

4 bali wale wenye busara walitwaa na mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.

5 Hatta bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala.

6 Hatta usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi anakuja; tokeni kwenda kumlaki.

7 Marra wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao.

8 Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.

9 Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakinena, Labuda hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia kwenda kwao wauzao, mkanunue wenyewe.

10 Nao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja nae arusini: mlango ukafungwa.

11 Khalafu wakaja na wale wanawali wengine, wakinena, Bwana, Bwana, utufungulie.

12 Akajibu, akasema, Amin, nawaambieni, siwajui ninyi.

13 Bassi kesheni, maana hamwijui siku wala saa ajapo Mwana wa Adamu.

14 Maana ni mfano wa mtu atakae kusafiri kwenda inchi ya ugeni, aliwaita watumishi wake, akaweka kwao mali zake.

15 Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; killa mtu kwa kadri ya uwezo wake; marra akasafiri.

16 Bassi yule aliyepokea talanta tano akashika njia, akafanya kazi nazo, akachuma talanta nyingine tano.

17 Vilevile na yule mwenye mbili, yeye nae akachuma nyingine mbili faida.

18 Bali yule aliyepokea moja, alikwenda akafukua chini, akaiticha fedha ya bwana wake.

19 Baada ya siku nyingi yuaja bwana wa watumishi wale, akafanya hesabu nao.

20 Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akinena, Bwana, uliweka kwangu talanta tano: tazama, talanta nyingine tano zaidi nilizopatafaida.

21 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema, na amini: ulikuwa amini kwa machache, nitakuweka juu ya mengi: ingia katika furaha ya bwana wako.

22 Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili: tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida.

23 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema na amini: ulikuwa amini kwa machache, nitakuweka juu ya mengi: ingia katika furaha ya bwana wako.

24 Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya:

25 nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako chini ya inchi: tazama, unayo iliyo yako.

26 Bwana wake akajibu, akamwambia, Mtumishi mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;

27 bassi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwao wawekao fedha ya watu; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.

28 Bassi, mnyangʼanyeni talanta yake, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.

29 Kwa maana killa aliye na mali atapewa, na kuongezewa: nae asiye nayo, hatta ile aliyo nayo atanyangʼanywa.

30 Na mtumishi yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza ya nje; huko kutakuwa kilio na kusaga meno.

31 Hatta atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja nae, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake:

32 na mataifa yote watakusanyika mbele yake: nae atawabagua kama vile mchunga abaguavyo kondoo na mbuzi:

33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.

34 Kisha Mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa wa Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tangu kuumbwa ulimwengu:

35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;

36 nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.

37 Ndipo wenye haki watakaponijibu, wakinena, Bwana, lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?

38 Lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?

39 Lini tulipokuona u mgonjwa, an kifungoni, tukakujia?

40 Na mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambieni. Kadiri mlivyomtendea mmojawapo katika hawo ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.

41 Kisha atawaambia na wale walio mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, kwenda katika moto wa milele, aliowekewa tayari Shetani na malaika zake:

42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;

43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike: nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.

44 Ndipo hawo pia watajibu, wakinena, Bwana, lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikukhudumu?

45 Nae atawajibu, akinena, Amin, nawaambieni, Kadiri msivyomtendea mmojawapo katika hawo walio wadogo, na mimi hamkunitendea.

46 Na hawo watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele: bali wenye haki katika uzima wa milele.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo