Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 YESU akaenda zake, akatoka hekaluni; wanafunzi wake wakamwendea illi kumwonyesha majengo ya hekalu.

2 Yesu akajibu akawaambia, Hamyaoni haya yote? Amin, nawaambieni, Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitahomolewa.

3 Hatta alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakinena, Tuambie, haya yatakuwa lini? Na nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia?

4 Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganyeni.

5 Kwa maana wengi watakuja kwa jina langu, wakinena, Mimi ni Kristo; na watadanganya wengi.

6 Na mtasikia khabari za vita na uvumi wa vita: angalieni, msitishwe: maana haya hayana buddi kuwa; lakini mwisho wenyewe hado.

7 Maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwako na njaa, na maradhi, na matetemeko ya inchi pahali pahali.

8 Haya yote ni mwanzo wa utungu.

9 Wakati huo watawasaliti ninyi mpate kuteswa, na watawaua; na mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa vote kwa ajili ya jina langu.

10 Ndipo wengi watajikwaa, na watasalitiana, na kuchukiana.

11 Na manabii wengi wa uwongo wataondoka, watadanganya wengi.

12 Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, pendo la watu wengi litapoa.

13 Lakini astahimiliye hatta mwisho, ndiye atakaeokoka.

14 Na injili hii ya ufalme itakhubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; ndipo ule mwisho utakapokuja.

15 Bassi mlionapo chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama mahali patakatifu (asomae afahamu),

16 ndipo walio katika Yahudi wakimbilie milimani;

17 nae aliye juu ya nyumba asishuke avichukue vitu vilivyomo nyumbani mwake;

18 nae aliye mashamba asirudi nyuma azichukue nguo zake.

19 Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku zile!

20 Ombeni kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato.

21 Maana wakati ule itakuwapo shidda kubwa, jinsi isivyopata kuwa tangu mwanzo wa ulimweugu hatta leo, wala haitakuwa kamwe.

22 Na kama siku zile zisingalikatizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitakatizwa siku zile.

23 Wakati huo mtu akiwaambieni, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko huko, msisadiki.

24 Kwa maana wataondoka Makristo ya uwongo, na manabii ya uwongo, nao watafanyiza ishara kubwa ua mataajabu; wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wateule.

25 Angalieni, nimetangulia kuwaambieni.

26 Bassi wakiwaamhieni, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki.

27 Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hatta magharibi; hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

28 Maana po potemzoga utakapokuwapo, ndipo tai watakapokusanyika.

29 Marra baada ya shidda ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbingu zitatikisika:

30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni: ndipo mataifa yote ya ulimwengu wataomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbingu kwa nguvu pamoja na utukufu mwingi.

31 Nae atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya panda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande mmoja wa mwisho wa mbinguni mpaka upande wa pili.

32 Kwa mtini jifunzeni mfano: tawi lake likiisha kuwa laini na kuchanua majani, mwafahamu ya kuwa wakati wa hari ni karibu;

33 vivyo hivyo na ninyi, myaonapo haya yote, fahamuni ya kuwa yu karibu, tena milangoni.

34 Amin, nawaambieni, Hakitapita kizazi hiki, hatta yatakapokuwa haya yote.

35 Mbingu na inchi zitapita; bali maneno yangu hayatapita kamwe.

36 Na khabari ya siku ile na saa ile hakuna ajuae, hatta malaika walio mbinguni, illa, Baba yangu peke yake.

37 Lakini kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo na kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

38 Kwa maana kama vile siku ziie zilizokuwa kabla ya gharika watu walivyokuwa wakila, wakinywa, wakioa, wakioza, hatta siku ile aliyoingia Nuhu katika safina,

39 wasitambue, hatta gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo na kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

40 Wakati huo watu wawili watakuwa mashamba; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;

41 wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.

42 Kesheni bassi: kwa maana hamwijui saa atakayokuja Bwana wenu.

43 Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angalijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliacha nyumba yake kuvunjwa.

44 Kwa sababu hii na ninyi mwe tayari; kwa sababu saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.

45 Nani bassi aliye mtumishi yule amini mwenye haki, ambae bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape chakula kwa saa yake?

46 Yu kheri mtumishi yule, ambae bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivi.

47 Amin, nawaambieni, atamweka juu ya mali zake zote.

48 Bali mtumishi yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia;

49 nae akianza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi:

50 bwana wa mtumishi yule atakuja siku asiyotazamia, na saa asiyotambua,

51 atamkata vipande viwili, ataweka sehemu yake pamoja na wanafiki: ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo