Mathayo 23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 KIISHA Yesu akasema na makutano na wanafunzi wake, akinena, 2 Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa: 3 bassi, yo yote watakayowaambieni myashike; yashikeni na kuyatenda: lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende: maana hunena wala hawatendi. 4 Kwa maana hufunga mizigo mizito isiyochukulika na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuisogeza kwa kidole chao. 5 Tena matendo yao yote huyatenda illi kutazamwa na watu: hupanua fulakteria zao, huongeza matamvna ya mavazi yao; 6 hupenda mahali pa mbele katika karamu, na viti vya mbele katika sunagogi, 7 na kusalimiwa sokoni, na kuitwa na watu, Rabbi, Rabbi. 8 Bali ninyi nisiitwe Rabbi; maana mwalimu wenu yu mmoja ndiye Kristo, na ninyi nyote ni ndugu. 9 Wala msimwite mtu baba yenu duniani: maana Baba yeuu yu mmoja, aliye mbinguni. 10 Wala msiitwe wakufunzi; maana mkufunzi wenu yu mmoja, ndiye Kristo. 11 Nae aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu. 12 Na ye yote atakaejikuza, atadhiliwa; na ye yote atakaejidhili, atakuzwa. 13 Ole wenu waandisbi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapokea hukumu iliyo kubwa mno. 14 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, nao wanaoingia hamwaachi waingie. 15 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnazunguka katika bahari na inchi kavu illi kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehannum marra mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe. 16 Ole wenu viongozi vipofu, ninyi mnenao, Mtu atakaeapa kwa hekalu, si kitu; bali mtu atakaeapa kwa dhababu ya hekalu, amejifunga. 17 Wapumbavu ninyi na vipofu: maana ipi iliyo kubwa, ile dhahabu, au lile hekalu liitakasalo dhababu? 18 Tena, Mtu atakaeapa kwa madhbahu, si kitu; bali mtu atakaeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amejifunga. 19 Wapumbavu ninyi na vipofu; maana ipi kubwa, ile sadaka, au ile madhbahu iitakasayo sadaka? 20 Bassi yeye aapae kwa madhbahu, yuapa kwayo na kwa vitu vyote vilivyo juu yake. 21 Nae aapae kwa hekalu, yuapa kwalo, na kwa yeye akaae ndani yake. 22 Nae aapae kwa mbingu, yuapa kwa kiti cha Mungu, na kwa yeye akaae juu yake. 23 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnalipa zaka za mnaana na bizari na kumini, mkaacha mambo makuu ya sharia, hukumu, na rehema, na imani: haya imewapasa kuyafanya, na mengine yale msiyaache. 24 Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia. 25 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa nmasafisha nje ya kikombe na chungu, na ndani yake vimejaa unyangʼanyi na kutoa kuwa na kiasi. 26 Ewe Farisayo kipofu, takasa kwanza ndani ya kikombe na chungu, illi nje yake nayo ipate kuwa safi. 27 Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa yamepambwa, bali kwa ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote. 28 Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, hali kwa ndani mmejaa unafiki na maasi. 29 Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki? kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki, 30 na kunena, Kama sisi tungalikuwako zamani za haha zetu, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii. 31 Hivi mwajishuhudia nafsi zenu, ya kwamba ninyi ni wana wao waliowana manabii. 32 Kajazeni kipimo cha baba zenu. 33 Enyi nyoka, mazao wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehannum? 34 Kwa sababu hii, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi: na wengine wao mtawaua na mtawasulibi, na wengine wao mtawapiga katika sunagogi zenu, na mtawafukuza mji kwa mji; 35 illi iwajieni damu yote ya haki iliyomwagika katika inchi, tangu damu ya Habil, yule mwenye haki, hatta damu ya Zakaria, mwana wa Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhbahu, 36 Amin, nawaambieni, Mambo haya yote yatakijia kizazi hiki. 37 Ee Yerusalemi, Yerusalemi, wenye kuwaua manabii, na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! marra ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hamkukubali! 38 Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa tupu. 39 Kwa maana nawaambieni, Hamtaniona kamwe tangu leo, hatta mtakaposema, Ameharikiwa ajae kwa jina la Bwana. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania