Mathayo 22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 YESU akajibu, akawaambia tena kwa mifano, akinena, 2 Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwana wake arusi. 3 Akawatuma watumishi wake wawaite walioalikwa kuja arusini: nao hawakutaka kuja. 4 Akatuma tena watumishi wengine, akinena, Waambieni wale walioalikwa, Tʼazameni nimeandaa karamu yangu: ngʼombe na vinono vimekwisha kuehinjwa, na vyote vimekuwa tayari, njoni arusini. 5 Lakini hawakujali, wakaenda zao, mmoja shambani kwake, mmoja kwenye biashara yake: 6 nao waliosalia wakawakamata watumishi wake, wakawatenda jeuri, wakawana. 7 Bassi yule mfalme alipopata khahari, akaghadhabika: akapeleka majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao. 8 Kisha akawaambia watumishi wake. Arusi i tayari, lakini wale walioalikwa hawakustahili. 9 Bassi enendeni hatta njia panda za njia kuu, na wote mwaonao waiteni arusini. 10 Watumishi wale wakatoka wakaingia njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu na wema: arusi ikajaa wageni. 11 Alipoingia yule mfalme kuwatazama wageni, akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la arusi. 12 Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? Akatekewa. 13 Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni miguu na mikono, mchukueni mkamtupe katika giza la nje: ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno. 14 Kwa maana wengi waitwao, wateule wachache. 15 Ndipo Mafarisayo wakaenda zao, wakafauya shauri, jinsi ya kumtega kwa maneno. 16 Wakawatuma kwake wanafunzi wao pamoja na Maherodiano, wakanena, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, ua njia va Mungu waifundisha katika kweli, wala hujali cheo cha mtu, kwa maana hutazami sura za watu. 17 Bassi utuambie, Waonaje? Ni halali kumpa Kaisari kodi, au si halali? 18 Lakini Yesu akaufahamu uovu wao, akasema, Mbona mnanijaribu, enyi wanafiki? 19 Nionyesheni fedha ya kodi. Nao wakamletea dinari. 20 Akawaambia, Ya nani sanamu hii, na anwani hii? 21 Wakamwambia, Ya Kaisari. Akawaambia, Bassi, mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu. 22 Waliposikia, wakataajabu, wakamwacha, wakaenda zao. 23 Siku ile Masadukayo, watu wanenao kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza, 24 wakinena, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, nae hana watoto, ndugu yake amwoe mkewe, illi ampatie ndugu yake mzao. 25 Bassi, kwetu palikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia ndugu yake nike wake. 26 Vivyo hivyo wa pili nae, na wa tatu, hatta wote saba. 27 Mwisho wa wote yule mwanamke akafa nae. 28 Katika kiyama, hassi, atakuwa mke wa nani katika wale saba? Maana wote walikuwa nae. 29 Yesu akajihu, akawaamhia, Mwajidanganya, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu. 30 Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaozwi, bali huwa kama malaika wa Mungu mbinguni. 31 Tena katika khabari ya kiyama ya wafu, hamjaiisoma neno lililonenwa na Mungu, akisema, 32 Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaak, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, hali wa wahayi. 33 Makutano waliposikia, wakashangaa kwa elimu yake. 34 Na Mafarisayo waliposikia ya kwamba amewafumba kinywa wale Masadukayo, wakakusanyika pamoja. 35 Mmoja wao, mwana sharia, akamwuliza, akimjaribu; akinena, 36 Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? 37 Yesu akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. 38 Amri ya kwanza na iliyo kuu ndiyo hii. 39 Na ya pili yafanana nayo, ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. 40 Amri hizi mbili yazitegemea torati yote nao manabii. 41 Mafarisayo walipokusanyika, Yesu akawauliza, 42 akinena, Mwaonaje katika khabari za Kristo? Yu mwana wa nani? Wakamwambia, Wa Daud. 43 Akawaambia, Imekuwaje bassi Daud katika Roho kumwita Bwana, akinena, 44 Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti mkono wangu wa kuume, Hatta niwawekapo adui zako chini ya miguu yako? 45 Bassi, Daud akimwita Bwana, amekuwaje mwana wake? 46 Hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu tangu siku ile kumwuliza neno tena. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania