Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 HATTA walipokaribia Yerusalemi, na kufika Bethfage, katika mlima wa Mizeituni, ndipo Yesu akatuma wanafunzi wawili,

2 akiwaambia, Enendeni zenu hatta kijiji kile kinachowakabili, na marra mtaona punda amefungwa, na mwana punda pamoja nae: mfungueni mkaniletee.

3 Na kama mtu akiwaambieni neno, semeni, Bwana ana haja nao; na marra moja atawapeleka.

4 Haya yote yamepata kuwa, illi litimie neno lililonenwa na nabii, akisema,

5 Mwambieni binti Sayuni, Tazama, mfalme wako anakuja kwako, Mpole, amepanda punda, Na mwana punda, mtoto wa punda.

6 Wale wanafunzi wakaenda zao, wakafanya kama Yesu alivyowaamuru,

7 wakamleta yule punda na mwana punda, wakaweka nguo zao juu yao, wakamketisha.

8 Watu wengi katika makutano wakatandaza nguo zao njiani; wengine wakikata matawi ya miti, wakiyatandaza njiani.

9 Na makutano waliotangulia, na waliofuata, wakapaaza sauti zao, wakinena, Utuokoe sasa, Mwana wa Daud; amebarikiwa ajae kwa jina la Bwana; Utuokoe sasa wewe uliye juu.

10 Hatta alipoingia Yerusalenn, mji wote ukataharuki, nkinena, Ni nani huyu?

11 Makutano wakanena, Huyu ni Yesu, yule nabii wa Nazareti ya Galilaya.

12 Yesu akaingia ndani ya hekalu la Mungu, akawafukuza wote waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwa wakiuza njiwa;

13 akawaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itakwitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyangʼanyi.

14 Vipofu na viwete wakamwendea hekaluni, akawaponya.

15 Lakini makuhani wakuu na waandishi walipoyaona maajabu aliyoyafanya, na watoto wakipaaza sauti zao hekaluni, wakinena, Utuokoe sasa, mwana wa Daud! wakakasirika,

16 wakamwambia, Wasikia hawa wanenavyo? Yesu akawaambia, Naam; hamkupata kusoma, Kwa vinywa vya watoto wachanga na wanyonyao umekamilisha sifa?

17 Akawaacha, akatoka nje ya mji mpaka Bethania, akalala huko.

18 Hatta assubuhi alipokuwa akirudi mjini, akashikwa na njaa.

19 Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake illa majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hatta milele. Mtini ukauyauka marra moja.

20 Wanafunzi wake walipoona, wakastaajabu, wakinena, Umenyaukaje mtini marra moja?

21 Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambieni, Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hatta mkiuambia mlima huu, Ngʼoka, ukatupwe baharini, itatendeka.

22 Na yo yote mtakayoyaomba katika kusali, mkiamini, mtapokea.

23 Hatta alipokwisha kuingia hekaluni, makuhani wakuu na wazee wa watu wakamwendea alipokuwa akifundisha, wakinena, Kwa mamlaka gani unafanya haya? Na nani aliyekupa mamlaka haya?

24 Yesu akajibu, akawaambia, Nami nitawaulizeni neno moja; mkinijibu, nami nitawaambieni, kwa mamlaka gani ninafanya haya.

25 Ubatizo wa Yohana ulitoka wapi? Ulitoka mbinguni, au kwa wana Adamu? Wakasemezana wao kwa wao, wakinena, Tukisema, Ulitoka mbinguni; atatuambia, Mbona bassi hamkumwamini?

26 Na tukisema, Kwa wana Adamu; twaogopa makutano; maana watu wote wanaona ya kuwa Yohana ni nabii.

27 Wakamjibu Yesu, wakasema, Hatujui. Nae akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi kwa mamlaka gani ninafanya haya.

28 Mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na watoto wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo enenda kufanya kazi katika shamba langu la mizabibu.

29 Akajibu akasema, Sitaki; baadae akatubu, akaenda.

30 Akamwendea yule wa pili, akasema vilevile. Nae akajibu akasema, Nakwenda, Bwana: asiende.

31 Katika hawa wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya baba yake? Wakamwambia, Yule wa kwanza. Yesu akawaambia, Amin, nawaambieni, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu.

32 Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, nanyi hamkumwamini; lakini watoza ushuru na makahaha walimwamini: nanyi mlipoona, hamkutuhu haada ya haya, na kumwamini.

33 Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, nae alipanda mizabibu, akazungusha uzio, akachimba shimo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.

34 Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumishi wake kwa wale wakulima, wajiokee matunda yake.

35 Wale wakulima wakawakamata watumishi wake, huyu wakampiga, na mwingine wakamwua, na mwingine wakampiga mawe.

36 Akatuma tena watumishi wengine wengi kuliko wa kwanza, wakawatenda vilevile.

37 Baadae akamtuma mwanawe kwao, akinena, Mwana wangu watamjali.

38 Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake.

39 Wakamkamata, wakamtupa uje ya shamba la mizabibu, wakamwua.

40 Bassi atakapokuja yule bwana wa mizabibu, atawatendea nini wale wakulima?

41 Wakamwambia, Atawaangamiza wabaya wale; nae atawapangisha mizabibu wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake.

42 Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hili lilikuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu?

43 Kwa sababu hii nawaambieni, ya kwamba ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, na watapewa taifa lingine wenye kuzaa matunda yake.

44 Nae aangukiae juu ya jiwe hili atavunjikavunjika: nae amhae litamwangukia, litampondaponda.

45 Makuhani wakuu na Mafarisayo, waliposikia mifano yake, wakatambua ya kuwa anawanena wao.

46 Nao walipotafuta kumkamata, wakawaogopa makutano, kwa maana walimwona kuwa nabii.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo