Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 20 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 KWA maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba, aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu.

2 Na alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, akawapeleka katika shamba lake la mizabibu.

3 Akatoka muamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi;

4 na hawo nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo liaki nitakupeni. Wakaenda.

5 Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vilevile.

6 Hatta mnamo saa edashara akatoka, akakuta wengine wakisimama wasiokuwa na kazi, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?

7 Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, Enendeni na ninyi katika shamba la mizabibu, na iliyo haki mtapata.

8 Kulipokuchwa, yule bwana wa mizabibu akamwambia msimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe ijara yao, ukianzia wa mwisho hatta wa kwanza.

9 Walipokuja wale wa saa edashara, wakapokea killa mtu dinari.

10 Na wale wa kwanza walipokuja, wakadhani watapokea zaidi; na wao pia wakapokea killa mtu dinari.

11 Wakiisha kupokea, wakamnungʼunikia mwenye nyumba,

12 wakinena, Hawa wa mwisho wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana.

13 Nae akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa dinari?

14 Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe.

15 Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu nipendavyo? Au jicho lako ni ovn kwa sababu ya kuwa mimi mwema?

16 Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza wa mwisho: maana waitwao wengi, hali wateule wachache.

17 Hatta Yesu alipokuwa akipanda kwenda Yerusalemi, aliwachukua wanafunzi thenashara kwa faragha njiani, akawaambia,

18 Angalieni, tunapanda kwenda Yerusalemi; na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa makuhani wakuu na waandishi; nao watamhukumu afe;

19 na watampeleka kwa Mataifa wapate kumdhihaki, na kumpiga mijeledi, na kumsulibi; na siku ya tatu atafufuka.

20 Ndipo mama ya wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akimsujudia, akimwomba neno.

21 Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, Agiza hawa wanangu waketi mmoja mkono wako wa kunme; na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako.

22 Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomha. Mwaweza kuuywea kikombe nitakachonywea mimi, na kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi? Wakamwambia, Twaweza.

23 Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu, na mtabatizwa ubatizo nibatizwao mimi; lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri niwapeni, bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu.

24 Na wale kumi waliposikia, wakawakasirikia wale ndugu wawili.

25 Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wafalme wa Mataifa huwatawala, na wakuu wao huwatumikisha.

26 Lakini kwemi ninyi haitakuwa hivi: bali ye yote atakae kuwa mkuu kwenu, na awe mkhudumu wenu;

27 na ye yote atakae kuwa wa kwanza kwenu awe mtumishi wenu:

28 kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kukhudumiwa, bali kukhudumu, na kutoa roho yake kuwa dia ya wengi.

29 Hatta walipokuwa wakitoka Yeriko mkutano mkubwa wakamfuata.

30 Na vipofu wawili wameketi kando ya njia, nao waliposikia ya kwamba Yesu anapita, wakapaaza sauti zao, wakinena, Uturehemu, Ee Bwana, mwana wa Daud!

31 Makutano wakawakaripia, wanyamaze. Lakini wao wakazidi kupaaza sauti zao, wakinena, Uturehemu, Ee Bwana, mwana wa Daud!

32 Yesu akasimama, akawaita, akasema, Mnataka niwafanyie nini?

33 Wakamwambia, Bwana, macho yetu yafumbuliwe.

34 Yesu akawahurumia, akawagusa macho yao; marra macho yao yakapata kuona, wakamfuata.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo