Mathayo 2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 ALIPOZALIWA Yesu katika Bethlehemu ya Yahudi zamani za mfalme Herode, majusi wa mashariki walifika Yerusalemi, 2 wakinena, Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyola yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudu. 3 Mfalme Herode aliposikia haya, akafadhaika, na Yerusalemi pia pamoja nae. 4 Akakusanya makuhani wakuu wote na waandishi wa watu, akatafuta khabari kwao, Kristo azaliwa wapi? 5 Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Yahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii, 6 Na wewe Bethlehemu wa inchi ya Yuda, Huwi mdogo kamwe katika majumbe ya Yuda: Kwa kuwa kwako atatoka liwali Atakaewachunga watu wangu Israeli. 7 Kisha Herode akawaita majusi kwa faragha, akapata kwao hakika ya muda ile nyota ilipoonekana. 8 Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkahoji sana mambo ya mtoto; mkiisha kumwona, nileteeni khabari, illi nami nije nimsujudie. 9 Nao waliposikia maneno ya mfalme wakashika njia; na tazama ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hatta ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto. 10 Walipoiona ile nyota, wakafurahi furaha kuliwa mno. 11 Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mama yake, wakaanguka wakasujudu; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tumi, dhahabu, uvumba, na manemane. 12 Nao wakiisha kuonywa katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine. 13 Na hawo walipokwisha kwenda zao, malaika wu Bwami akamtokea Yusuf katika ndoto, akiuena, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukakae huko mpaka nikuambiapo; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize. 14 Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake hatta Misri; 15 akawa huko mpaka alipokufa Herode: illi litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema, Kutoka Misri nalimwita mwaua wangu. 16 Bassi Herode, akiona ya kuwa amedhihakiwa na majusi, akaghadhabika sana, akatuma watu kuwaua watoto wote wanawaume waliokuwa Bethlehemu na viungani mwake mwote, tangu wa miaka miwili na waliopungua, kwa muda aliouhakiki kwa majusi. 17 Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema, 18 Sauti ilisikiwa Rama, Kilio, na kulalama, na maombolezo, Rahel akiwalilia watoto wake, Asikubali kufarijiwa, maana hawako. 19 Hatta alipofariki Herode, malaika wa Bwana akamtokea Yusuf katika ndoto huko Misri, akinena, 20 Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ushike njia kwenda inchi ya Israeli: kwa maana wamekufa walioilafuta roho ya mtoto. 21 Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake, akatika inchi ya Israeli. 22 Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki Yahudi mahali pa Herode baba yake, akaogopa kwenda huko; akaonywa katika ndoto, akaenda zake hatta pande za Galilaya, 23 akaenda, akakaa mji uliokwitwa Nazareti: illi litimie neno lililonenwa na manabii, Atakwitwa Mnazorayo. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania