Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 IKAWA Yesu alipomaliza maneno haya, akatoka Galilaya akafika mipaka ya Yahudi, ngʼambu ya Yordani.

2 Makutano mengi wakamfuata, akawaponya huko.

3 Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je, ni halali mtu kumwacha mkewe kwa killa sababu?

4 Akajihu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,

5 akasema. Kwa sababu hii, mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe; na hawo wawili watakuwa mwili mmoja?

6 Hatta wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Bassi alivyoviunganisha, Mungu, mwana Adamu asivitenganishe.

7 Wakamwambia, Jinsi gani bassi Musa aliamuru kumpa khati ya talaka, na kumwacha?

8 Akawaambia, Musa kwa sabau ya ugumu wa mioyo yenu aliwapeni ruksa kuwaacha wake zenu: lakini langu mwanzo haikuwa hivi.

9 Nami nawaambia ninyi, Killa mtu atakaemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya asharati, akaoa mwingine, azini; nae amwoae yule aliyeachwa azini.

10 Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa liivi, haifai kuoa.

11 Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, illa wale waliojaliwa.

12 Maana wako matawashi waliozaliwa katika hali hii toka matumboni mwa mama zao; teua wako matawashi waliofanywa kuwa matawashi na watu: tena wako matawashi waliojifanya kuwa matawashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezae kulipokea neno hili, na alipokee.

13 Ndipo akaletewa vitoto aweke mikono yake juu yao na kuwaombea; wanafunzi wake wakawakemea.

14 Lakini Yesu akasema, Waacheni vitoto, wala msiwakataze kuja kwangu; kwa maana walio mfano wa hawo, ufalme wa mbinguni ni wao.

15 Akaweka mikono yake juu yao, akatoka huko.

16 Mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu mwema, nitende jambo gani jema, illi nipate uzima wa milele?

17 Akamwambia, Ya nini kuniita mwema? Hakuna mwema illa mmoja, ndiye Mungu. Lakini ukitaka kuingia katika nzima, zishike amri.

18 Akamwambia, Zipi? Yesu akasema, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudu uwongo,

19 Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako.

20 Yule kijima akamwambia, Haya yote nimeyashika tangu utoto wangu: nimepmigukiwa nini tena?

21 Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze mali zako, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kiisha njoo unifuate.

22 Yule kijana alipolisikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali mengi.

23 Yesu akawaambia wanafunzi wake, Amin, nawaambieni, ya kwamba itakuwa shidda tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni.

24 Nawaambieni tena, Ni rakhisi ngamia kupenya katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.

25 Wanafunzi wake waliposikia, wakashangaa sana, wakinena, Nani bassi awezae kuokoka?

26 Yesu akawatazama, akawaambia, Kwa wana Adamu hili haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.

27 Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata: tutapata nini bassi?

28 Yesu akamwambia, Amin, nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata, katika zamani za kuzaliwa upya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti thenashara, mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli.

29 Na killa mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea marra mia, na kurithi uzima wa milele.

30 Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho, wa kwanza.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo