Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 SAA ile wanafunzi wakamwendea Yesu wakinena, Ni nani bassi aliye mkuu kafika ufalme wa mbinguni?

2 Yesu akaita kitoto, akamweka katikati yao,

3 akasema, Amin, nawaambieni, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kabisa katika ufalme wa mbinguni.

4 Bassi, ye yote anyenyekeae kama kitoto hiki, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.

5 Na ye yote atakaepokea kitoto kimoja mfano wa hiki kwa jina langu, anipokea mimi:

6 bali atakaekosesha mmoja wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungwe jiwe kubwa la kusagia shingoni mwake, na kutoswa katika kilindi cha bahari.

7 Ole wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana buddi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletae jambo la kukosesha!

8 Mkono wako au mguu wako ukikukosesha, ukate, ukautupe mbali nawe; ni vyema zaidi kuingia katika uzima umepungukiwa mkono au mguu, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele.

9 Na jicho lako likikukosesha, lingʼoe, ukalitupe mbali nawe; ni vyema zaidi kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jebannum ya moto.

10 Angalieni msidharau mmoja wa wadogo hawa; kwa maana nawaambieni ya kwamba malaika zao mbinguni siku zote wanamtazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.

11 Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea.

12 Mwaonaje? mtu akiwa na kondoo mia, mmoja akampotea, je, hawaachi wale tissa na tissaini, akaenda milimani, na kumtafuta yule aliyepotea?

13 Hatta akipata kumwona, amin nawaambieni, amfurahia huyu zaidi, kuliko wale tissa na tissaini wasiopotea.

14 Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni mmoja wa wadogo hawa apotee.

15 Na ndugu yako akikutenda dhambi, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu: akikusikia, umempata ndugu yako.

16 La, hakusikia, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, illi kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu killa neno lithubutike.

17 Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa: na asipolisikiliza kanisa pia, na awe sawasawa na mtu wa Mataifa na mtoza ushuru.

18 Amin, nawaambieni, Yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.

19 Tena nawaambieni, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.

20 Kwa kuwa wawili au watatu walipo wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.

21 Kiisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu akinitenda dhambi nimsamehe marra ngapi? hatta marra saba?

22 Yesu akamwumbia, Sikuambii hatta marra saba, bali hatta marra sabaini fi saba.

23 Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumisbi wake.

24 Alipoanza kuifanya, akaletewa mtu mmoja awiwae nae talanta elfu kumi.

25 Na asipokuwa na kitu cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni.

26 Bassi yule mtumishi akaanguka, akamsujudia akinena, Bwana, niwie kwa saburi, nami nitakulipa vyote pia.

27 Bwana wa mtumishi yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni.

28 Mtumishi yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyewiwa nae dinari mia; akamkamata, akamshika koo, akinena, Nilipe uwiwacho.

29 Bassi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akinena, Niwie kwa saburi, nami nitakulipa vyote pia.

30 Nae hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hatta atakapoilipa ile deni.

31 Bassi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, wakasikitika sana, wakaenda wakamfafanulia bwana wao yote yaliyotendeka.

32 Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumishi mwovu, nalikusamehe deni ile yote, uliponisihi:

33 nawe, je, haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?

34 Bwana wake akaghadhabika, akampeleka kwa watesaji, hatta atakapoilipa deni ile yote.

35 Vivyo hivyo na Baba yangu wa mbinguni atawatenda ninyi, kama ninyi kwa mioyo yenu hamkusamehe killa mtu ndugu yake makosa yake.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo