Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 WAKAMJIA Mafarisayo na Masadukayo, wakamjaribu, wakamwomba awaonyeshe ishara itokayo mbinguni.

2 Akajibu, akawaambia, Kukichwa, mwanena, Kutakuwa na kianga: kwa maana uwingu ni mwekundu.

3 Na assubuhi, Leo dhoruba; kwa maana uwingu ni mwekundu, na kumetanda. Enyi wanafiki, mnajua kuutamhua uso wa uwingu; hali ishara za zamani hizi hamziwezi.

4 Kizazi kibaya na cha zina chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya nabii Yunus. Akawaacha, akaenda zake.

5 Wanafunzi wake wakaenda hatta ngʼambu, wakasahau kuchukua mikate.

6 Yesu akawaambia, Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Masudukayo.

7 Wakabishana wao kwa wao, wakinena, Ni kwa sababu hatukuchukua mikate.

8 Yesu akajua, akawaambia, Mbona mnabishana ninyi kwa ninyi, enyi wa imani haba, kwa sababu hamkuchukua mikate?

9 Hamjafahamu hado, wala hamkumbuki ile mikate mitano kwa wale elfu tano, na vikapu vingapi mlivyookota?

10 Wala ile mikate saba kwa wale elfu nne, na makanda mangapi mliyookota?

11 Imekuwaje hamkufahamu ya kuwa si kwa sababu ya mkate naliwaambieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo?

12 Ndipo wakafahamu ya kuwa hakuwaambia kujihadhari na chachu ya mkate, bali elimu ya Mafarisayo na Masadukayo.

13 Yesu akaenda pande za Kaisaria Filipi, akawauliza wanafunzi wake akinena, Watu huninena mimi, Mwana wa Adamu, kuwa nani?

14 Wakasema, Wengine Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.

15 Akawaambia, Na ninyi mwaninena mimi kuwa nani?

16 Simon Petro akajibu, akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hayi.

17 Yesu akajibu, akamwambia, U kheri Simon bar Yunus; kwa kuwa nyama na damu hazikukufunulia haya, bali Baba yangu aliye mbinguni.

18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na jun ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; na milango ya kuzimu haitalishinda.

19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litafungwa mbinguni: na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.

20 Ndipo akawaagiza sana wanafunzi wake wasimwambie mtu ya kwamba yeye ndiye Yesu aliye Kristo.

21 Toka wakati huo Yesu akaanza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemi, na kuteswa mengi na wazee na makuhani wakuu, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.

22 Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akinena, Hasha, Bwana, haya hayatakupata.

23 Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u chukizo kwangu: maana huyawazi mambo ya Mungu, bali yaliyo ya wana Adamu.

24 Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu atakae kuandama nyuma yangu, ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake, anifuate.

25 Maana mtu atakae kuisalimisha roho yake, ataiangamiza; na mtu atakaeitoa roho yake kwa ajili yangu, ataiona.

26 Kwa maana atafaidiwa mtu nini akiupata ulimwengu wote, na kupata khasara ya roho yake? au mtu atatoa nini badala ya roho yake?

27 Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atamlipa killa mtu kwa kadiri ya kutenda kwake.

28 Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawo wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hatta watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo