Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 NDIPO waandishi na Mafarisayo toka Yerusalemi wakamwendea Yesu wakinena,

2 Mbona wanafunizi wako huyakhalifu mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula.

3 Akajibu, akawaambia, Mbona na ninyi huikhalifu amri ya Mungu kwa mapokeo yenu?

4 Kwa kuwa Mungu aliamuru, akisema, Mheshimu baba yako na mama yako; na, Amtukanae baba yake au mama yake na afe.

5 Bali ninyi hunena, Afakaemwambia baba yake au mama yake, Cho chote kikupasacho kufaidiwa nami ni sadaka, asimheshimu baba yake au mama yake, huwa bassi.

6 Mkalitangua neno la Mungu kwa mapokeo yemi.

7 Enyi wanafiki, ni vyema alivyotabiri Isaya katika khabari zenu, akinena,

8 Watu hawa hunikaribia kwa vinywa vyao, Na kwa midomo yao huniheshimu; Bali mioyo yao iko mbali yangu.

9 Nao waniabudu ibada ya burre. Wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wana Adamu.

10 Akawaita makutano akawaambia, Sikieni, mfahamu:

11 Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho najis mwana Adamu; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho najis mwana Adamu.

12 Ndipo wanafunzi wake wakamwendea, wakamwambia, Wajua ya kuwa Mafarisayo walipolisikia neno lile walichukizwa?

13 Akajibu, akasema, Killa pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni, litangʼolewa.

14 Waacheni hawo; ni vipofu, viongozi wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumhukia shimoni wote wawili.

15 Petro akajibu, akamwambia, Tueleze mfano huo. Yesu akasema,

16 Hatta na ninyi mngali hamna akili?

17 Hamjafahamu bado ya kuwa killa kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni?

18 Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo najis mwana Adamu.

19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, mauaji, mazini, asharati, uizi, ushuhuda wa uwongo, na matukano;

20 hayo ndiyo yamtiayo najis mwana Adamu; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mwana Adamu najis.

21 Yesu akatoka huko, akaenda pande za Turo na Sidon.

22 Na mwanamke Mkauanaya wa mipaka ile akatokea, akampaazia sauti, akinena, Unirehemu. Bwana, Mwana wa Daud; binti yangu amepagawa sana na pepo.

23 Nae hakumjibu neno. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakinena. Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.

24 Nae akajibu, akasema, Sikupelekwa illa kwa kondoo zilizopotea za nyumba ya Israeli.

25 Nae akaja akamsujudia, akinena. Bwana, nisaidie.

26 Akajibu akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.

27 Akasema, Ndio, Bwana, illakini hatta mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao.

28 Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Ee mwanamke, imani yako kubwa; pata utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.

29 Yesu akapita huko, akafika kando ya bahari ya Galilaya; akapanda mlimani, akaketi huko.

30 Wakamwendea makutano mengi walio na viwete, vipofu, bubu, vilema, na wengine wengi pamoja nao, wakawaweka miguuni pa Yesu; akawaponya;

31 hatta makutano wakastaajabu, walipowaona bubu wanasema, vilema wanakuwa wazima, viwete wanakwenda, na vipofu wanaona; wakamtukuza Mungu wa Israeli.

32 Yesu akawaita wanafunzi wake, akasema, Nawahurumia makutano, kwa kuwa yapata siku tatu wamekaa pamoja nami, hawana kitu cha kula: na kuwaaga wakifunga sitaki, wasije wakazimia njiani.

33 Wanafunzi wake wakamwambia, Tupate wapi mikate mingi hapa nyikani, hatta kushibisha makutano mengi namna hii?

34 Yesu akawaambia, Mikate mingapi mnayo? Wakasema, Saba, na visamaki vichache.

35 Akawaagiza makutano waketi chini:

36 akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru, akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano.

37 Wakala wote wakashiba: wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, makanda saba, yamejaa.

38 Nao waliokula walikuwa wanaume elfu nne, bila wanawake na watoto.

39 Akawaaga makutano, akapanda chomboni, akaenda pande za Magdala.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo