Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 WAKATI ule Yesu alipita katika makonde siku ya sabato; wanafunzi wake wakaona njaa, wakaanza kuvunja masuke, wakala.

2 Na Mafarisayo walipoona, wakamwambia, Tazama! wanafunzi wako wanatenda lililo haramu kutenda siku ya sabato.

3 Akawaambia, Hamkusoma alivyotenda Daud, alipokuwa na njaa, yeye na wenzi wake;

4 jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaila mikate iliyotolewa kwa Mungu, isiyo halali kuliwa nae wala na wenzi wake, illa na makuhani peke yao?

5 Wala hamkusoma katika torati, kwamba siku ya sabato makuhani hekaluni huinajisi sabato wasipate khatiya?

6 Lakini nawaambieni, kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu.

7 Kama mngalijua maana ya maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka, hamngaliwalaumu wasio na khatiya.

8 Kwa maana Mwana wa Adamu udiye Bwana wa sabato.

9 Akaondoka huko, akaiugia katika sunagogi lao.

10 Na tazama mtu mwenye mkono umepooza, wakamwuliza, wakinena, Ni halali kuponya watu siku ya sabato? wapate kumshtaki.

11 Akawaambia, Ni mtu yupi miongoni mwenu mwenye kondoo mmoja, yule kondoo akatumbukia shimoni siku ya sabato, asiyemshika akamwondosha?

12 Je! mtu si hora sana kuliko kondoo? Bassi ni halali kutenda mema siku ya sabato.

13 Akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako; akaunyosha, ukapona, nkawa mzima kama mkono wa pili.

14 Lakini Mafarisayo wakatoka wakamfanyia shauri la kumwangamiza.

15 Nae Yesu akijua haya akatoka huko: makutano mengi wakamfuata; akawaponya wote,

16 akawaagiza wasimdhihirishe;

17 illi litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,

18 Tazama, mtumishi wangu niiliyemteua; Mpendwa wangu, ambae moyo wangu umependezwa nae; Nitamtia roho yangu, Nae atuwatangazia Mataifa hukumu.

19 Hatateta, wala hatapaaza sauti yake; Wala mtu hatasikia sauti yake njiani.

20 Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala kitani kitokacho moshi hatakizima, Hatta aletapo hukumu yake ikashinda.

21 Na jina lake Mataifa watalitumainia.

22 Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu na bubu; akamponya, hatta yule kipofu na bubu akasema na kuona.

23 Makutano wote wakashangaa wakasema, Huyu siye mwana wa Daud?

24 Lakini Mafarisayo waliposikia, wakasema, Huyu hafukuzi pepo, illa kwa uweza wa Beelzebul mkuu wa pepo.

25 Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Killa ufalme ukifitinika na nafsi yake, hufanyika ukiwa; na killa mji au nyumba ikifitinika na nafsi yake, haitasimama.

26 Na Shetani akimfukuza Shetani, amefitinika na nafsi yake; bassi ufalme wake utasimamaje?

27 Na mimi nikifukuza pepo kwa uweza wa Beelzebul, je! wana wenu wawafukuza kwa uweza wa nani? Kwa sababu hii hawo ndio watakaokuwa waamuzi wenu.

28 Lakini mimi nikifukuza pepo kwa uweza wa Bobo ya Mungu, bassi ufalme wa Mungu umekujieni.

29 Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? ndipo atakapoiteka nyumba yake.

30 Mtu asiye upande wangu yu kinyume changu; na mtu asivekusanya pamoja nami hutapanya.

31 Kwa sababu hii nawaambieni, Killa dhambi na killa neno la kufuru watasamehewa wana Adamu, bali kumtukana Roho hawatasamehewa wana Adamu.

32 Na killa mtu atakaenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakaenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ntakaokuwa.

33 Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hujulikana.

34 Uzao wa nyoka, mwawezaje kusema mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.

35 Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa mema: na mtu mbaya katika hazina yake mbaya hutoa mabaya,

36 Bassi, nawaambieni, Killa neno lisilo maana, watakalolisema wana Adamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.

37 Maana kwa maneno yako utapewa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.

38 Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakinena, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako.

39 Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zina chataka ishara, wala hakitapewa ishara, ilia ishara ya nabii Yunus.

40 Maana kama vile Yunus alivyokuwa siku tatu mchana na nsiku katika tumbo la nyamgumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa inchi.

41 Watu wa Ninawi watasimama siku ile ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watakihukumu: maana wao walitubu kwa makhubiri ya Yunus; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yunus.

42 Malkia wa kusini ataondoka siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nae atakihukumu: maana yeye alikuja kutoka pande za mwisho za ulimwengu asikie hekima ya Sulemani; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.

43 Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupita kati ya pahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.

44 Khalafu hunena, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa.

45 Marra huenda, akachukua pamoja nae pepo wengine saba walio waovu kupita nafsi yake, nao huingia na kukaa humo; na mambo, ya mwisho ya mtu yule huwa mabaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kiovu.

46 Alipokuwa katika kusema na makutano, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wakitaka kusema nae.

47 Mtu akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe.

48 Akajihu, akamwambia yule aliyempa khabari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni nani?

49 Akawanyoshea mkono wanafunzi wake, akasema. Tazama, Mama yangu na ndugu zangu!

50 Kwa maana ye yote atakaeyafanya mapenzi ya baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo