Mathayo 11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 IKAWA Yesu alijiokwisha kuwaagiza wanafunzi wake thenashara, akatoka huka kwenda kufundisha na kukhubiri katika miji yao. 2 Nae Yohana aliposikia huko gerezani matendo yake Kristo, alituma wawili katika wanafunzi wake, kumwambia, 3 Wewe ndiye ajae, au tumtazamie mwingine? 4 Yesu akajibu akawaambia, Enendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona: 5 vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanakhubiriwa khabari njema. 6 Na yu kheri ye yote asiyechukiwa nami. 7 Nao wakienda zao, Yesu akaanza kuwaambia makutano khabari za Yohana, Mlitoka kwenda jangwani kutazama nini? Unyasi ukilikiswa na upepo? 8 Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi meroro? Watu wavaao mavazi meroro, wamo katika nyumba za wafalme. 9 Lakini mlikwenda kuona nini? Nabii? Naam, nawaambieni, na aliye zaidi ya nabii. 10 Kwa maana huyo ndiye aliyeandikiwa, Tazama, mimi namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako. Atakaeitengeneza njia yako mbele yako. 11 Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji: illakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye. 12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hatta leo ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka. 13 Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana. 14 Na ikiwa mantaka kukubali, yeye ndiye Elia atakaekuja. 15 Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie. 16 Nitafananisha na nini kizazi hiki? Kimefanana na watoto wakikaa sokoni, wanaowaita wenzao, 17 wakinena, Twaliwapigia filimbi, wala hamkucheza; twaliomboleza, wala hamkulia. 18 Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakanena. Yuna pepo. 19 Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakanena, Mlafi huyu, na mnywa mvinyo, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imepewa haki na watoto wake. 20 Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu haikutubu. 21 Ole wako, Korazin! Ole wako, Bethsaida! Kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Turo na Sidon, wangalitubu zamani kwa kuvaa gunia na majivu. 22 Lakini, nawaambieni, itakuwa rakhisi Turo na Sidon istahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi. 23 Nawe Kapernaum, uliyeinuliwa hatta mbinguni, utashushwa hatta kuzimu: kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwako, ingalifanyika katika Sodom, ungalikuwapo hatta leo. 24 Lakini nawaambieni, itakuwa rakhisi inchi ya Sodom istahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe. 25 Wakati ule Yesu akajibu akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa uliwaficha haya wenye hekima na busara, ukawafunulia wadogo: 26 Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele yako. 27 Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu: wala hakuna mtu amjuae Mwana, illa Baba; wala hakuna mtu amjuae Baba illa Mwana, na ye yote ambae Mwana apenda kumfunulia. 28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye mizigo nami nitawapumzisha. 29 Jitieni nira yangu, jifunzeni kwa mfano wangu; kwa kuwa mimi ni mpole na moyo wangu umenyenyekea: nanyi mtapata raha rohoni mwenu; 30 kwa maana nira yangu laini, na mzigo wangu mwepesi. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania