Mathayo 10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 AKAWAITA wanafunzi wake thenashara, akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu, wawafukuze, na kuponya magonjwa yote na dhaifu zote. 2 Na majina ya mitume thenashara ni haya: Wa kwanza Simon aliyekwitwa Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobo wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake; 3 Filipo, na Bartolomayo, na Tomaso, na Mattayo mtoza ushuru; Yakobo wa Alfayo, na Lebbayo, aliyekwitwa Thaddayo; 4 Simon Kananayo, na Yuda Iskariote, ndiye aliyemsaliti. 5 Hawa thenashara Yesu aliwatuma, akawaagiza, akinena, Katika njia ya Mataifa msiende, wala mjini mwa Wasamaria msiingie: 6 afadhali shikeni njia kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. 7 Na katika kuenenda kwenu, khubirini, nikinena, Ufalme wa mbinguni umekaribia. 8 Ponyeni wagonjwa, takaseni wenye ukoma, fufueni wafu, fukuzeni pepo; mmepata burre, toeni burre. 9 Msichukue dhahabu, wala fedha, wala shaba mishipini mwenu; 10 wala mkoba wa safari, wula kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo: maana mtenda kazi astahili posho lake. 11 Na mji wo wote au kijiji cho chote mtakachoingia, tafuteni ni nani humo aliye mtu amini; kakaeni humo hatta mtakapotoka. 12 Na mkiingia katika nyumba, isalimuni. 13 Na nyumba ile ikistahili, amani yenu iifikilie: la, haistahili, amani yenu iwarudieni. 14 Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kungʼuteni mavumbi ya miguuni mwenu. 15 Amin, nawaambieni, Itakuwa rakhisi inchi ya Sodoma na Gomora istahimili adhabu yao siku ya hukumu, kuliko mji ule. 16 Angalieni, mimi nawatumeni kama kondoo kati ya mbwa wa mwitu: bassi mwe na busara kama nyoka, na msio na dhara kama hua. 17 Jihadharini na wana Adamu; kwa maana watawapelekeni mbele ya baraza, na katika masunagogi yao watawapiga; 18 nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, illi kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa. 19 Lakini hapo wakatapowapelekeni, msifikirifikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema. 20 Kwa kuwa si ninyi msemao, bali Roho ya Baba yenu asemae ndani yenu. 21 Na ndugu atamsaliti ndugu apate kufa, na baba atamsaliti mtolo; na watoto wataondoka kuwashitaki wazee wao, wawafishe. 22 Na mtakuwa mkichukiwa na watu wole kwa ajili ya jina langu: lakini adumuye hatta mwisho, ndiye atakaeokoka. 23 Watakapowaudhi katika mji huu, kimbilieni mwingine: kwa maana ni kweli nawaambieni, Hamtaimaliza miji yote ya Israeli, hatta ajapo Mwana wa Adamu. 24 Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, wala mtumishi hampiti bwana wake. 25 Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebul, je, si zaidi wale walio nyumbani mwake? 26 Bassi, msiwaogope, kwa maana hakuna jambo lililostirika, ambalo halitafunuliwa baadae; wala lililofichwa, ambalo halitajulikana baadae. 27 Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni kalika nuru; na msikialo kwa siri, likhubirini juu ya nyumba. 28 Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho: afadhali mmwogopeni yule awezae kuangamiza mwili na roho pia katika jehannum. 29 Videge viwili haviuzwi kwa pesa moja? Na hatta mmoja haanguki chini asijiojua Baba yemi: 30 hatta na nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. 31 Msiogope bassi; hora ninyi kuliko videge vingi. 32 Bassi killa mtu atakaenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni. 33 Bali mtu ye yote atakaenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni. 34 Msidhani ya kuwa nalikuja kueneza amani duniani; la! sikuja kueneza amani, bali upanga. 35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na baba yake, na binti na mama yake, na mkwe na mkwe mtu: 36 na adui wa mtu ndio wale wa nyumbani mwake. 37 Apendae baba au mama kuliko mimi, hanifai; na apendae mwana au binti kuliko mimi hanifai. 38 Nae asiyechukua msalaba wake na kufuata nyuma yangu, hanifai. 39 Anaeipata roho yake ataiangamiza; nae anaeitoa roho yake kwa ajili yangu ataipata. 40 Awapokeae ninyi, anipokea mimi; nae anipokeae mimi, ampokea yeye aliyenituma. 41 Ampokeae nabii kwa kuwa yu nabii, atapata thawabu ya nabii; nae ampokeae mwenye haki kwa kuwa yu mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki. 42 Na mtu aliye yote atakaemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa kikombe cha maji ya baridi tu, kwa kuwa yu mwanafunzi, amin, nawaambieni, haitampotea kamwe thawabu yake. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania