Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 NA Saul alikuwa akiona vema auawe. Siku ile kukatukia adha nyingi juu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemi: wote wakatawanyika katika inchi ya Yahudi na Samaria, illa mitume.

2 Watu watawa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo mengi.

3 Saul akaliharibu kanisa, akiingia killa nyumba, na kuwabarura wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani.

4 Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilikhubiri neno.

5 Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria, akawakhubiri Kristo.

6 Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yote yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuiona miujiza aliyokuwa akiifanya.

7 Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu: na watu wengi waliopooza, na viwete, wakaponywa.

8 Ikawa furaha kubwa kafika mji ule.

9 Na mtu mmoja, jina lake Simon, alikuwa amefanya uchawi katika mji ule tokeapo, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa.

10 Wote wakamsikiliza kwa muda mwingi, tangu mdogo hatta mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni nweza wa Mungu, ule mkuu.

11 Wakamwangalia, kwa maana muda mwingi amewashangaza kwa uchawi wake.

12 Lakini walimpomwamini Filipo, akizikhubiri khabari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.

13 Na yeye Simon mwenyewe aliamini akabatizwa, akakaa na Filipo: akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka.

14 Na mitume walioko Yerusalemi, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana.

15 Wakashuka, wakawaombea wrampokee Roho Mtakatifu:

16 kwa maana bado hajawashukia hatta mmoja wao, illa wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu.

17 Wakaweka mikono yao juu yao, nao wakapokea Roho Mtakatifu.

18 Hatta Simon alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekwa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha, akisema,

19 Nipe na mimi uwezo huu, illi killa mtu nitakaemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu.

20 Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhani ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali.

21 Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele ya Mungu.

22 Bassi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana illi, kama yumkini, usamebewe fikara lui ya moyo wako.

23 Kwa maana nakuona una nchungu kama nyongo, na tena u katika kifungo cha uovu.

24 Simon akajibu, akasema, Niombeeni ninyi kwa Mungu, yasinifikilie mambo haya uliyosema.

25 Nao walipokwisha kushuhudia na kulikhubiri neno la Bwana wakarudi Yerusalemi wakaikhubiri Injili katika vijiji vingi vya Wasamaria.

26 Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka uende upande wa kusini hatta njia ile itelemkayo kutoka Yemsalemi kwenda Gaza; nayo ni jangwa.

27 Akaondoka, akaenda; marra akamwona mtu wa Ethiopia, tawashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkiya wa Ethiopia, aliyewekwa juu ya hazina yake yote;

28 nae amekwenda Yerusalemi kuabudu, akawa akirejea, ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya.

29 Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari bili, ukashikamane nalo.

30 Bassi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya: akanena, Je, yamekuelea haya unayosoma?

31 Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiougoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja nae.

32 Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili: Alichukuliwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana kondoo asivyolia mbele yake amkatae manyoya, Vivyo hivyo yeve nae hafunui kinywa chake.

33 Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa. Ni nani atakaeeleza kizazi chake? Kwa maana uzima wake umeondolewa katika inchi.

34 Yule tawashi akamjibu Filipo, Nakuomba, nabii huyu asema maneno haya kwa khabari ya nani; ni khabari zake mwenyewe an khabari za mtu mwingine?

35 Filipo akafunua kinywa chake na akilianzia andiko hili, akamkhubiri khabari njema za Yesu.

36 Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji: yule tawashi akasema, Yanizuia nini nisibatizwe?

37 Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, ni halali. Akajibu, akanena, Namwamini Mwana wa Mungu kuwa ndiye Yesu Kristo.

38 Akaamuru lile gari lisimame: wakatelemka wote wawili majini. Filipo na yule tawashi: akambatiza.

39 Kiisha, walipotoka majini, Roho ya Bwana ikamnyakua Filipo, yule tawashi asimwone tena; maana alikwenda zake akifurahi:

40 Filipo akaonekana katika Azoto, na alipokuwa akipita akakhubiri Injili katika miji yote, hatta akafika Kaisaria.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo