Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 HATTA siku ziie wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manungʼuniko ya Wahelenisti juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika khuduma ya killa siku.

2 Wale thenashara wakawaita jamii va wanafunzi, wakasema, Haipendezi sisi kuliacha neno la Mungu na kukhudumu mezani.

3 Bassi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, illi tuwaweke juu ya jambo hili:

4 na sisi tutadumu katika kumwomba Mungu na kulikhudumia Neno lake.

5 Neno hili likapendeza machoni jia mkutano wote: wakamehagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu na Filipo, na Prokoro, na Nikanor, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia.

6 Wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao.

7 Nenu la Mungu likaenea: hesahu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemi: jamii kubwa la makuhani wakaitii Imani.

8 Na Stefano, akijaa imani na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu.

9 Lakini baadhi ya watu wa sunagogi lililokwitwa sunagogi la Malibertino, na la Wakurene na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka wakajadiliana na Stefano:

10 lakini hawakuweza kushindana na hekima yake wala na Roho aliyosema nayo.

11 Hatta wakashawishi watu waliosema, Tumemsikia mtu huyu akinena maneno ya kumtukana Musa na Mungu.

12 Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi: wakaniwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza.

13 Wakasimamisha mashahidi wa uwongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kufuru juu ya mahali hapa patakatifu na juu ya torati:

14 maana tumemsikia akisema kwamba Yesu huyo Mnazareti atapaharibu pahali hapa, na kuzihadili desturi tulizopewa na Musa.

15 Watu wote walioketi katika ile baraza wakamkazia macho yao, wakamwona uso wake kuwa kama uso wa malaika.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo