Matendo 5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 LAKINI mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza uwanja, 2 akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe nae akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume. 3 Petro akamwambia, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo kumwambia uwongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya uwanja? 4 Ulipokuwa kwako, haukuwa mali yako? Na ulipokuwa umekwisha kuuzwa haukuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hatta ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uwongo mwana Adamu, bali Mungu. 5 Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Khofu nyiugi ikawapata watu wote walioyasikia haya. 6 Vijana wakaondoka, wakamtia katika saanda, wakamchukua nje, wakamzika. 7 Hatta muda wa saa tatu baadae mkewe akaingia, nae hana khabari ya hayo yaliyotokea. 8 Petro akamjibu, Niambie, Mliuuza uwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndio, kwa thamani hiyo. 9 Petro akamwambia, Hikuwaje hatta mkapatana kumjaribu Roho ya Bwana? angalia, miguu yao waliomzika mume wako ipo mlangoni, nao watakuchukua wewe nawe. 10 Marra akaanguka miguuni pake akafa: wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe. 11 Khofu nyingi ikawapata kanisa lote na watu wote walioyasikia haya. 12 Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu: nao wote walikuwa kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani: 13 na katika wote wengine hapana hatta mmoja aliyethubutu kuambatana nao: illa watu waliwaadhimisha: 14 waamini wakazidi kuja kwa Bwana, wengi, wanaume ha wanawake: 15 hatta katika njia kuu hutoa nje wagonjwa, huwaweka juu ya mifarashi na vitanda, illi, Petro akija, kivuli chake tu kimtie kivuli mmojawapo wao. 16 Nayo makutano ya miji ilioyo kando kando ya Yerusalemi yakakutanika, wakileta wagonjwa, nao walioudhiwa na pepo wachafu: nao wote wakaponywa. 17 Akaondoka kuhani mkuu na wote waliokuwa pamoja nae (hao ndio walio wa madhehehu ya Masadukayo) wamejaa wivu, 18 wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza; 19 lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema, 20 Enendeni mkasimame hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya uzima huu. 21 Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha. Akaja kuhani mkuu nao walio pamoja nae, wakawaita watu wa haraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani illi wawalete. 22 Hatta watumishi walipofika hawakuwaona gerezani, 23 wakarudi wakatoa khabari, wakisema, Gereza tumeikuta imefungwa salama salamini, nao walinzi wamesimama mbele ya mlango: lakini tuliponfungua hatukukuta mtu ndani. 24 Kuhani mkuu na jemadari wa hekalu na makuhani wakuu waliposikia haya, wakaingiwa na mashaka kwa ajili yao, yatakuwaje mambo hayo. 25 Mtu mmoja akaja akawapasha khabari ya kama, Watu wale mliowaweka gerezani wako ndani ya hekalu, wamesimama wakiwafundisha watu. 26 Yule jemadari akaenda pamoja na watumishi, wakawaleta, lakini si kwa nguvu, kwa maana waliogopa watu wasije wakawatupia mawe. 27 Wakawaleta, wakaweka katika baraza. Kuhani mkuu akawauliza, akisema, 28 Je! hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili: nanyi mmeijaza Yerusalemi mafundisho yenu, na mnataka kuleta damu ya mtu yule juu yetu. 29 Petro na mitume wakajibu, wakaaena, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wana Adamu. 30 Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, ambae ninyi mlimwua mkamtundika katika mti. 31 Mtu kuyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toha na masamaha ya dhambi. 32 Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambae Mungu amewapa wote wamtiio. 33 Waliposikia wakachomwa mioyo yao; wakafanya shauri kuwaua. 34 Lakini mtu mmoja, Farisayo, jina lake Gamaliel, mwalimu wa torati, mwenye kuheshimiwa na watu wote, akasimama katika baraza, 35 akaamuru mitume wawekwe nje kitambo, akawaambia, Enyi waume wa Israeli, jihadharini jinsi mtakavyowatenda watu hawa. 36 Kwa sababu kabla ya siku hizi aliondoka Theuda, akidai ya kuwa yeye ni mtu, mkuu watu wapata aroba mia wakashikamana nae, na wote waliomsadiki wakatawanyika wakawa si kitu. 37 Baada ya mtu huyo aliondoka Yuda Mgalilaya, siku zile za kuandikiwa kodi, akawavuta watu kadha wa kadha nyuma yake, nae akapotea na wote waliomsadiki wakatawanyika. 38 Bassi sasa nawaambieni, Jiepusheni na watu hawa, waacheni: kwa kuwa shauri hili au kazi hii ikiwa ya kibinadamu, itavunjwa, 39 illakini ikiwa ya Mungu hamwezi kuivunja; msije mkaonekana kuwa mnapigana na Mungu. 40 Wakakubali maneno yake; wakawaita mitume, wakawapiga, wakawaamuru wasinene kwa jina lake Yesu; kiisha wakawaacha waende zao. 41 Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya jina lake. 42 Na killa siku ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kukhubiri khabari njema za Yesu kwamba ni Kristo. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania