Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 HATTA walipokuwa wakisema na watu wale, makuhani na akida wa hekalu na Masadukayo wakawatokea,

2 wakifadhaika sana kwa sababu wanawafundisha watu na kuukhubiri ufufuo wa wafu unaopatikana kwa Yesu.

3 Wakawakamata, wakawaweka garezani hatta assubuhi; kwa kuwa imekwisha kuwa jioni.

4 Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini: na hesabu ya watu ilikuwa kama elfu tano.

5 Hatta assubuhi wakubwa na wazee na waandishi wakakusanyika Yerusalemi,

6 na Kayafa pia, na Yohana, na Iskander, na wo wote waliokuwa jamaa zake kuhani mkuu.

7 Wakawaweka katikati, wakawauliza, Kwa nguvu gani na kwa jina la nani mmefanya haya ninyi?

8 Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia,

9 Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli, kama tukiulizwa leo khabari ya yule mtu dhaifu jinsi alivyoponywa,

10 jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Mnazareti, ambae ninyi mlimsulibisha, Mungu akamfufua, kwa jina hilo mtu huyu anasimama mzima mbele yenu.

11 Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni.

12 Wala hakuna wokofu katika mwingine aliye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wana Adamu litupasalo kuokolewa nalo.

13 Bassi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kujua ya kuwa ni watu wasio elimu, wasio maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.

14 Na wakimwona yule aliyeponywa akisimama pamoja nao hawakuwa na neno la kujibu.

15 Wakawaamuru kutoka katika baraza, wakafanya shauri, wakisemii, Tuwafanyieni watu hawa?

16 maana ishara mashuhuri imefanywa nao, iliyo dhabiri kwa watu wote wakaao Yerusalemi, wala hatuwezi kuikana.

17 Lakini neno hili lisije likaenea katika watu, tuwaogofishe wasiseme tena na mtu aliye yote kwa jina hili.

18 Wakawaita, wakawaagiza wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu.

19 Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia,

20 Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.

21 Nao walipokwisha kuwaogofya tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu: kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa hayo yaliyotendeka:

22 maana umri wake yule mtu aliyefanyiwa ishara hii ya kuponya ulipita miaka arubaini.

23 Hatta walipofunguliwa, wakaenda kwa watu wao, wakawapasha khabari ya mambo yote waliyoambiwa na makuhani wakuu na wazee.

24 Nao waliposikia, wakampaazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na inchi na bahari na vitu vyote vilivyomo:

25 nawe ulinena kwa kinywa cha Daud mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na watu wametafakari ubatili?

26 Wafalme wa dunia wamejipanga, Na wakuu wamefanya shauri pamoja, Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake.

27 Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika juu ya mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,

28 illi wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee.

29 Bassi sasa, Bwana, yaangalie maogofya yao; ukawajalie watumishi wako kunena neno lako kwa uthabiti,

30 ukinyosha mkono wako kuponya: ishara na maajabu zifanyike kwa jina la mtumishi wako mtakatifu Yesu.

31 Hatta walipokwisha kumwomba Mungu, pahali paie walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa uthabiti.

32 Na jamii ya watu walioamini walikuwa moyo mmoja na roho moja: wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika.

33 Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa uguvu nyingi. Neema nyingi ikawa juu yao wote.

34 Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na uwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa

35 wakaiweka miguuni jia mitume; killa mtu akagawiwa kwa kadiri alivyohitaji.

36 Na Yusuf, aliyeitwa na mitume Barnaba (tafsiri yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kupro,

37 alikuwa na shamba akaliuza, akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo