Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BASSI Petro na Yohana walikuwa wakipanda pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tissa.

2 Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mama yake alichukuliwa na watu, wakamweka killa siku katika mlango wa hekalu nitwao Mzuri, illi aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu.

3 Mtu huyu akiwaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka.

4 Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi.

5 Akawaangalia, akitaraja kupewa kitu nao.

6 Petro akanena, Fedha sina, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Mnazareti, simama uende.

7 Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, marra nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikapata nguvu.

8 Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda: akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka, akimsifu Mungu.

9 Watu wote wakamwona akieuda, akimsifu Mungu.

10 Wakamtambua, ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa ameketi na kuomba sadaka penye mlango mzuri wa hekalu: wakajaa ushangao wakastaajabia mambo yale yaliyompata.

11 Bassi yule kiwete aliyeponywa alipokuwa akiwashika Petro na Yohana, watu wote wakawakusanyikia mbio katika tao lile lililokwitwa tao la Sulemani; wakishangaa sana.

12 Hatta Petro alipoona haya akawajibu watu, Enyi Waisraeli, mbona mnastaajabia haya, au mbona mnatukazia macho sisi, kana kwamba tumemfanya huyu aende kwa nguvu zetu sisi, au kwa utawa wetu sisi?

13 Mungu wa Ibrahimu na Isaak na Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambae ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe.

14 Ninyi mlimkana yule Mtakatifu, yule Mwenye haki, mkataka mpewe muuaji:

15 mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambae Mungu amemfufua: na sisi tu mashahidi wake.

16 Na kwa imani ya jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnaemwona na kumjua: na imani ile iliyo kwa njia yake yeye imempatia huyu mbele yemi ninyi nyote uzima huu mkamilifu.

17 Bassi sasa ndugu, najua ya kuwa mliyatenda haya kwa kutokujua kwenu, kama na wakuu wenu walivyotenda.

18 Lakini mambo yale aliyokhubiri Mungu tangu zamani kwa vinywa vya manabii wake wote, ya kama Kristo atateswa, ameyatimiza hivyo.

19 Tubuni bassi, mrejee, illi dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuhurudishwa kwa kuwako kwake Bwana:

20 apate kumtuma Kristo aliyekhubiriwa kwenu tangu zamani;

21 ambae ilimpasa kupokewa mbinguni hatta zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa vinywa vya manabii wake tokea mwanzo wa ulimwengu.

22 Kwa maana Musa aliwaambia baba zetu ya kama, Bwana Mungu atawainulieni nabii, atakaetoka katika ndugu zenu, kama mimi, msikieni yeye katika mambo yote atakayonena.

23 Na itakuwa ya kwamba kilia mtu asiyemsikiliza nabii huyo ataangamizwa na kutengwa na watu wake.

24 Naam, na manabii wote tangu Samwil na wale waliokuja nyuma yake, wote walionena, walikhubiri khabari za siku hizi.

25 Ninyi m watoto wa manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu aliagana na baba zenu, akimwambia Ibrahimu, Katika uzao wako kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa.

26 Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, illi kuwabarikini kwa kumwepusha killa mmoja wenu na maovu wake.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo