Matendo 28 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 TULIPOKWISHA kuokoka, ndipo tukajua ya kuwa kisiwa kile chaitwa Melita. 2 Washenzi wakatufanyia fadhili zisizokuwa za kawaida. Kwa maana walikoka moto, wakatukaribisha sote, kwa sababu ya mvua iliyokunywa na kwa sababu ya baridi. 3 Paolo alipokuwa amekusanya mzigo wa kuni, na kuuweka juu ya moto, nyoka akatoka kwa ajili ya ule moto, akamzingisha katika mkono wake. 4 Washenzi walipomwona yule nyoka akimwangikia mkono, wakaambiana, Hakosi mtu huyu ni muuaji; na ijapokuwa ameokoka katika bahari, haki haimwachi kuishi. 5 Lakini yeye akamtikisia motoni asipate madhara. 6 Wakamwangalia sana wakidhani ya kuwa atavimba au kuanguka chini, amekwisha kufa kwa ghafula; na wakiisha kumwangalia sana, na kuona kwamba halimpati dhara lo lote, wakabadili fikara zao, wakasema kwamba yeye ni Mungu. 7 Karibu na mahali pale palikuwa na mashamba ya mkubwa wa kisiwa, jina lake Publio; mtu huyu akatukaribisha kwa moyo wa urafiki, akatufanya wageni wake kwa muda wa siku tatu. 8 Ikawa baba yake Publio alikuwa hawezi homa na kuhara damu. Paolo akaingia kwake, akaomba, akaweka mikono yake juu yake, akamponya 9 Yalipokwisha kutendeka hayo wengine waliokuwa na magonjwa katika kisiwa wakaja wakaponywa; nao wakatuheshimu kwa heshima nyingi. 10 Na tulipoondoka wakatupakilia vitu vile tulivyokuwa na haja navyo. 11 Baada ya miezi mitatu tukasafiri katika merikebu ya Iskanderia iliyokuwa imekaa pale kisiwani wakati wa baridi; na alama yake ni Dioskuri. 12 Tukafika Surakusa, tukakaa siku tatu. 13 Kutoka huko tukazunguka tukafikia Regio: baada ya siku moja upepo wa kusi ukavuma, na siku ya pili tukawasili Puteoli. 14 Huko tukakuta ndugu, tukasihiwa nao tukae siku saba; na hivi tukafika Rumi. 15 Na kutoka huko ndugu, waliposikia khabari zetu, wakaja kutulaki mpaka Appiiforo na Trestaberne. Paolo alipowaona akamshukuru Mungu, akachangaʼmka. 16 Tulipoingia Rumi akida akawatia wafungwa katika mikono ya jemadari wa walinzi wa Praitorio: bali Paolo alipewa rukhusa kukaa kwake mwenyewe pamoja na askari aliyemlinda. 17 Ikawa baada ya siku tatu akawaita wakuu wa Wayahudi wakutane; hatta walipokuja akawaambia, Wanaume ndugu, ningawa sikufanya neno kinyume cha watu wetu wala neno lililopingamana na desturi za baba zetu, nalitiwa katika mikono ya Warumi, nimefungwa, tokea Yerusalemi. 18 Na hao walipokwisha kuniuliza walitaka kunifungua, kwa maana hapakuwa na sababu yo yote ya kuuawa kwangu. 19 Lakini Wayahudi walipotoa hoja juu ya shauri hili nalishurutishwa kutaka rufaani kwa Kaisari. Si kwamba nalikuwa na neno la kuwashitaki watu wa taifa langu. 20 Bassi kwa ajili ya hayo, nimewaiteni mje kunitazama na kusema nami; kwa maana nimefungwa kwa mnyororo huu kwa ajili ya tumaini la Israeli. 21 Wale wakamwambia, Sisi hatukupata nyaraka zenye khabari zako kutoka Yahudi, wala hapana ndugu hatta mmoja aliyefika hapa na kutupasha khabari, au kunena neno baya juu yako. 22 Lakini tunataka kusikia kwako uonavyo wewe; kwa maana katika khabari za madhehebu hiyo tumekwisha kujua kwamba inanenwa vibaya kilia mahali. 23 Wakiislia kuwekana kwa siku, wakaja kwake nyumbani kwake, watu wengi sana, akawaeleza kwa taratibu na kuushuhudia ufalme wa Mungu, akiwaonya mambo yake Yesu, kwa maneno ya sharia ya Musa na ya manabii, tangu assubuhi hatta jioni. 24 Wengine waliamini yaliyonenwa, wengine hawakuyaamini. 25 Na walipokuwa hawapatani wao kwawao, wakaenda zao, Paolo alipokwisha kusema neno hili moja ya kama, Roho Mtakatifu alinena vema na baba zetu, kwa kinywa cha nabii Isaya, 26 Enenda kwa watu hawa, ukawaamhie, Kusikia, mtasikia wala hamtafahamu; Na kuona mtaona, wala hamtapata kujua neno: 27 Kwa maana mioyo ya watu hawa imepumbaa, Na masikio yao ni wazito wa kusikia, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Na kusikia kwa masikio yao, Na kufahamu kwa mioyo yao, Na kuhadili nia zao Nikawaponya. 28 Bassi ijulikane kwenu ya kwamba wokofu huu wa Mungu umepelekwa kwa mataifa, nao watasikia. 29 Alipokwisha kusema haya, Wayahudi wakaenda zao, wakiulizana mengi wao kwa wao. 30 Paolo akakaa muda wa miaka miwili mizima katika nyumba yake aliyokuwa ameipanga, akawakaribisha watu wote waliokuwa wakimwendea, akikhubiri khabari za ufalme wa Mungu, na kuwafundisha watu mambo ya Bwana Yesu Kristo, kwa ujasiri mwingi, asikatazwe na mtu. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania