Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 ENYI wanaume, ndugu zangu ua baba zangu, nisikilizeni, nikijitetea nafsi yangu mbele yemi sasa.

2 Waliposikia kwamba anasema nao kwa lugha ya Kiebrania wakazidi kunyamaza: akanena,

3 Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, nikalelewa katika niji huu miguumi pa Gamaliel, nikafundishwa sharia ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa ijtihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi:

4 nikawaudhi watu wa Njia hii kiasi cha kuwaua, nikawafunga, nikiwatia gerezani, wanaume na wanawake.

5 Kama kuhani mkuu nae anishuhudiavyo, na wazee wa baraza wote pia, ambao nalipewa barua nao kwa ndugu zao, nikaenda Dameski, illi niwalete wale waliokuwa huko hatta Yerusalemi, wamefungwa waadhibiwe.

6 Ikawa nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski, wakati wa adhdhuhuri, ghafula nuru kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote.

7 Nikaanguka chini, nikasikia sauti ikiniambia, Saul, Saul, Mbona unaniudhi?

8 Nikajibu Wewe nani Bwana? Akaniambia, Mimi ni Yesu Mnazareti, ambae wewe unaniudhi.

9 Na wale waliokuwa pamoja nami waliiona ile nuru, wakaingia khofu, illakini hawakuisikia ile sauti.

10 Nikasema, Nifanye nini, Bwana? Bwana akaniambia, Simama, uende hatta Dameski, na huko utaambiwa khabari za mambo vote yaliyoamriwa uyafanye.

11 Na nilipokuwa sioni kwa sababu ya fakhari ya nuru ile, nikaongozwa na mikono yao waliokuwa pamoja nami, nikafika Dameski.

12 Bassi mtu mmoja, Anania, mcha Mungu kwa kuifuata sharia, aliyeshuhudiwa na Wayahudi wote waliokaa huko, akanijia, akasimama karibu nami, akaniambia, Ndugu, Saul, uone.

13 Nikamwinulia macho yangu saa ile ile.

14 Akasema, Mungu wa baba zetu amekuchagua upate kujua mapenzi yake, na kumwona Mwenye haki, na kuisikia sauti itokayo katika kinywa chake.

15 Kwa maana utakuwa shahidi wake kwa watu wote, wa mambo hayo uliyoyaona na kuyasikia.

16 Bassi sasa, unakawiliani? Simama ubatizwe ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina la Bwana.

17 Ikawa nilipokwisha kurudi Yerusalemi, nilipokuwa nikisali ndani ya hekalu, nikawa katika hali ya rohoni,

18 nikamwona akiniambia, Hima, toka katika Yerusalemi upesi, kwa sababu hawatakubali ushuhuda wako katika khabari zangu.

19 Nami nikasema, Bwana, wanajua hao ya kuwa mimi nalikuwa nikwafunga wale wanaokuamini na kuwapiga katika masunagogi yao.

20 Na damu ya Stefano shahidi wako ilipomwagwa, mimi nami nilikuwa nikisimama karibu, nikikubali auawe, nikizitunza nguo zao waliomwua.

21 Nae akaniambia, Enenda zako; kwa kuwa mimi nitakutuma mbali kwa watu wa mataifa.

22 Wakamsikiliza mpaka neno lile, wakapaaza sauti zao, wakisema, Mwondoe huyu katika inchi, kwa maana haifai aishi.

23 Walipokuwa wakipiga kelele na kutupa mavazi yao na kurusharusha mavumbi juu,

24 yule jemadari akaamuru aletwe ndani ya ngome, akisema aulizwe khabari zake kwa kupigwa, illi ajue sababu hatta wakampigia kelele namna hii.

25 Hatta walipokwisha kumfunga kwa kamba, Paolo akamwambia akida aliyesimama karibu, Je! ni halali kumpiga mtu Mrumi nae hajahukumiwa bado?

26 Yule akida aliposikia, akaenda akamwarifu yule jemadari, akisema, Unataka kufanya nini? kwa maana mtu huyu ni Mrumi.

27 Jemadari akaja, akamwambia, Niambie, u Mrumi? Akasema, Ndio.

28 Jemadari akajibu, Mimi nalipata wenyeji huu kwa ras-il-mali nyingi. Paolo akasema, Na mimi nalizaliwa katika hali hiyo.

29 Bassi wale waliokuwa tayari kumwuliza wakaondoka wakamwacha. Na yule jemadari nae akaogopa, alipojua ya kuwa ni Mrumi, na kwa sababu amemfunga.

30 Siku ya pili yake akitaka kujua hakika, ni kwa sababu gani ameshitakiwa na Wayahudi, akamfungua, akawaamuru makuhani wakuu na baraza yote waje. Akamleta Paolo chini, akamweka mbele yao.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo