Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 IKAWA tulipokwisha kujitenga nao ua kutweka, tukafika Koos kwa tanga moja, na siku ya pili yake tukafika Rodo na kutoka huko tukafika Patara,

2 tukapata merikebu itakayovuka hatta Foiniki tukapanda tukatweka.

3 Na tulipoona Kupro tukaiacha upande wa kushoto: tukasafiri hatta Shami tukashuka Turo. Kwa maana huko ndiko marikebu yetu itakakoshusha shehena yake.

4 Tukiisha kuwaona wanafunzi tukakaa huko siku saba, nao wakamwambia Paolo kwa uwezo wa Roho Mtakatifu asipande kwenda Yerusalemi.

5 Hatta tulipotimiza siku zile tukaondoka tukaenda zetu, na watu wote pamoja na wake zao na watoto wao wakatusindikiza hatta nje ya mji, wakapiga magoti pwani wakaomba:

6 na baada ya kuagana tukapanda merikebuni, nao wakarudi kwao.

7 Hatta tulipomaliza safari yetu kutoka Troa tukafika Ptolemai, tukawasalimu ndugu tukakaa kwao siku moja.

8 Assubuhi yake sisi tulifuatana na Paolo tukatoka, tukafika Kaisaria, tukaingia nyumbani mwa Filipo, Mwinjilisti, aliyekuwa mmoja wa wale saba, tukakaa kwake.

9 Mtu huyu alikuwa na binti wane, mabikira, waliotabiri.

10 Bassi tulipokuwa tukikaa huko siku nyingi, nabii mmoja jina lake Agabo akashuka kutoka Yahudi.

11 Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paolo akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemi watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa mataifa.

12 Bassi tuliposikia haya, sisi na watu wa mahali pale, tukamsihi asipande kwenda Yerusalemi.

13 Paolo akajibu, Mnafanyaje, kulia na kunivnnja moyo? kwa maana mimi, licha ya kufungwa tu, ni tayari hatta kuuawa katika Yerusalemi kwa ajili ya jina lake Bwana Yesu.

14 Alipokataa shauri letu, tukanyamaza, tukisema. Mapenzi ya Bwana na yatendeke.

15 Baada ya siku zile tukachukua vyombo vyetu tukapanda kwenda Yerusalemi.

16 Baadhi ya wanafunzi wa Kaisaria wakafuatana na sisi, wakachukua na Mnason, mtu wa Kupro, mwanafunzi wa zamani ambae ndiye tutakaekaa kwake.

17 Tulipolika Yerusalemi ndugu wakatukaribisha kwa furaha.

18 Hatta siku ya pili yake Paolo akaingia kwa Yakobo pamoja naswi, na wazee wote walikuwako.

19 Na baada ya kuwasalimu, akawaeleza mambo yote moja moja Mungu aliyotenda katika mataifa kwa khuduma yake.

20 Nao waliposikia wakamhimidi Mungu, wakamwambia, Ndugu yetu, unaona kwamba Wayahudi walioamini walivyo elfu nyingi, nao wote wana wivu sana kwa ajili ya torati.

21 Nao wameambiwa khabari zako, ya kwamba unawafundisha Wayahudi wote wakaao katika mataifa kumwacha Musa, ukiwaambia wasiwatahiri watoto wao, wala wasizifuate desturi.

22 Bassi, ni nini? Bila shaka mkutano hauna buddi kukutanika, kwa maana watasikia kwamba umekuja.

23 Bassi fanya neno hili tunalokuambia: Wako kwetu watu wane waliofungwa na nadhiri.

24 Chukua watu hao, ujitakase pamoja nao, na kuwagharimia illi wanyoe vichwa vyao, watu wote wapate kujua ya kuwa khabari zile walizoambiwa juu yako si kitu, bali wewe mwenyewe unaenenda vizuri na kuishika sharia.

25 Kwa khabari za watu wa mataifa walioamini, tumekwisha kutoa hukumu yetu, wsio wasishike neno linginelo illa kujilinda nafsi zao na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na kitu kilichosongwa, na uasharati.

26 Ndipo Paolo akawatwaa wanaume wale, na siku va pili yake akajitakasa nafsi yake pamoja nao, akaingia ndani ya hekalu, akitangaza khabari ya kutimiza siku za utakaso, hatta sadaka itolewe kwa ajili ya kilia mmoja wao.

27 Bassi zile siku saba zilipokuwa karibu kutimizwa, Wayahudi waliotoka Asia wakamwona ndani ya hekalu, wakawataharakisha watu wote, wakamkamata, wakapiga kelele, Enyi wanaume wa Israeli, saidieni.

28 Huyu ndiye mtu yule afundishae watu katika killa mahali kinyume cha taifa letu na torati na pahali hapa. Tena, zaidi ya haya, amewaingiza Wayunani katika hekalu, akapatia najis pahali hapa palakatifu.

29 Kwa maana wamemwona Trofimo Mwefeso, pamoja nae mjini, wakadhani ya kuwa Paolo amemwingiza katika hekalu.

30 Mji wote ukataharuki, watu wakakutanika mbio mbio, wakamkamata Paolo, wakamwokota, wakamtoa hekaluni; marra milango ikafungwa.

31 Na walipokuwa wakitafuta njia ya kumwua, khabari zikamfikilia jemadari wa kikosi ya kwamba mji Yerusalemi umechafuka, mji mzima.

32 Marra hiyo akatwaa askari na maakida, akawashukia mbio. Nao walipomwona jemadari na askari wakaacha kumpiga Paolo.

33 Kiisha jemadari akakaribia, akamshika, akaamuru afungwe kwa minyororo miwili: akauliza, Nani huyu? tena, amefanya nini?

34 Wengine katika makutano wakapiga kelele wakisema hivi, na wengine hivi. Bassi alipokuwa hawezi kupata hakika ya khabari kwa sababu ya zile kelele, akatoa amri aletwe ndani ya ngome.

35 Bassi alipolika darajani ilikuwa yeye kuchukuliwa na askari kwa sababu ya jeuri ya makutano.

36 Maana kundi kubwa la watu wakamfuata, wakipiga kelele, Mwondoe huyu.

37 Na Paolo alipokuwa anaingizwa ndani ya ngome, akamwambia jemadari, Nina rukhusa nikuambie neno? Nae akasema, Je! unajua Kiyunani?

38 Wewe si vnle Mmisri ambae kabla ya siku hizi aliwafitinisha wale watu elfu nne, walioitwa Wauaji, akawaongoza jangwani?

39 Paolo akasema, Mimi ni mtu wa Kiyahudi, mtu wa Tarso, mji wa Kilikia, mwenyeji wa mji usio mnyonge. Nakuomba, nipe rukhusa niseme na wenyeji hawa.

40 Bassi, alipompa rukhusa, Paolo akasimama madarajani, akawapunjia mkono wale wenyeji; na ilipokuwa kimya kabisa, akanena nao kwa lugha ya Kiebrania, akisema,

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo