Matendo 20 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 KISHINDO kile kilipokoma, Paolo akawaita wanafunzi akaagana nao, akaondoka aende zake hatta Makedonia. 2 Na, akiisha kupita pande zile na kuwafariji kwa maneno mengi, akafika Uyunani. 3 Alipokwisha kukaa huko miezi mitatu, Wayahudi wakamfanyyia vitimbi, alipotaka kwenda Sham kwa njia ya bahari: bassi akaazimu kurejea kwa ujia ya Makedonia. 4 Watu hawa wakafuataua nae mpaka Asia, Sopater Mberoya, na Aristarko na Sekundo, watu wa Thessalonika, na Gayo mtu wa Derbe, na Tukiko na Trofumo watu wa Asia. 5 Watu hao wamekwisha kutangulia wakatungojea Troa. 6 Sisi tukatweka baada ya siku ya mikate isiyotiwa chachu, tukatoka Filippi, tukawafikia Troa, safari ya siku tano, tukakaa huko siku saba. 7 Hatta siku ya kwanza ya juma, wanafunzi walipokusanyika illi kumega mkate, Paolo akawakhutubu, akaazimu kusafiri siku ya pili yake, akafuliza maneno yake mpaka nsiku wa manane. 8 Palikiuwa na taa nyingi katika orofa ile walipokuwa wamekusanyika. 9 Kijana mmoja, jina lake Eutuko, ameketi dirishani, akalemewa na usingizi, akaanguka toka orofa ya tatu: akainuliwa amekwisha kufa. 10 Paolo akashuka, akamwangukia, akamkumbatia, akasema, Msifanye ghasia, maana uzima wake ungalimo ndani yake. 11 Akapanda juu tena, akamega mkate, akala, akazidi kuongea nao hatta alfajiri, ndipo akaenda zake. 12 Wakamleta yule kijana, yu mzima, wakafarajika faraja kubwa sana. 13 Sisi tukatangulia kwenda merikebuni, tukasafiri hatta Asso, tukikusudia kumpokea Paolo huko: kwa maana ndivyo alivyoagiza, yeye mwenyewe akiazimu kwenda kwa miguu. 14 Alipotufikia huko Asso, tukampokea, tukafika Mitulene. 15 Tukatweka kutoka huko, na siku ya pili tukafika mahali panapokabili Kio: siku ya pili yake tukawasili Samos, tukakaa Trogullio, siku ya pili tukafika Mileto. 16 Kwa sababu Paolo amekusudia kupita Efeso merikebuni, asije akakawia katika Asia: kwa maana alikuwa akifanya haraka, akitaka kuwahi Yerusalemi siku ya Pentekote, kama ikiwezekana. 17 Toka Mileto Faolo akatuma watu kwenda hatta Efeso, akawaita wazee wa Kanisa. 18 Walipofika kwake, akawaambia, Ninyi mnajua tangu siku ya kwanza nilipokanyaga hapa Asia, jinsi nilivyokuwa kwenu wakati wote, 19 nikimtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote, na machozi, na majaribu yaliyonipata kwa hila za Wayahudi; 20 ya kuwa sikuficha neno lo lote liwezaio kuwafaeni, bali naliwaonyesha na kuwafundisha kwa wazi na nyumba kwa nyumba, 21 nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani toba iliyo kwa Mungu, na imani iliyo kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 22 Bassi, sasa angalieni, nashika njia kwenda Yerusalemi nimefungwa rohoni, nisijue mambo yatakayonikuta huko; 23 illa ya kuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na mateso yaningoja. 24 Lakini siyahesabu maisha yaugu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na khuduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Injili ya neema ya Mungu. 25 Na sasa mimi najua ya kuwa ninyi nyote niliowakhubirini ufalme wa Mungu, nikienda huko na huko, hamtaniona uso tena. 26 Kwa hiyo nawashuhudia wote siku hii ya leo, ya kuwa mimi sina khatiya kwa damu ya mtu aliye yote. 27 Kwa maana sikujiepusha na kuwakhubirini khabari ya shauri lote la Mungu. 28 Jiangalieni nafsi zenu, na kundi lote, ambalo Roho Mtakatifu aliwakabidhi mlisimamie, kanisa lake Mungu, alilojipatia kwa damu yake mwenyewe. 29 Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa za mwitu wakali watakuja kwenu, wasiliachie kundi: 30 tena katika baadhi yenu wataondoka watu, wakisema mapotofu, wawavute wanafunzi kwenda nyuma yao. 31 Kwa biyo kesheni, mkikumbuka kama miaka mitatu, usiku na mchana, sikuacha kumwonya killa mtu kwa machozi. 32 Bassi, sasa ndugu, nawawekeni katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, kwake yeye awezae kuwajengeni na kuwapeni urithi pamoja nao wote waliotakasika. 33 Sikutamani fedha, wala dhahabu, wala mavazi ya mtu. 34 Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono hii imetumika kwa mahitaji yangu na yao walio pamoja nami. 35 Nimewapeni mfano katika mambo yote ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapaseni kuwasaidia wasio na nguvu, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni kheri kutoa kuliko kupokea. 36 Alipokwisha kunena haya akapiga magoti, akaomba pamoja nao wote. 37 Wakalia sana wote, wakamwangukia Paolo shingoni, wakambusu, 38 wakihuzunika zaidi kwa sababu ya neno lile alilosema, ya kwamba hawatamtazama uso tena. Wakamsindikiza hatta merikebuni. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania