Matendo 2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 HATTA ilipotimia siku ya Pentekote walikuwako wote pamoja mahali pamoja. 2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kassi, ukaijaza nyumba yote walipokuwa wameketi. 3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyika, kama ndimi za moto uliowakalia killa mmoja wao. 4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha mbalimbali, kama Roho alivyowajalia kutamka. 5 Na walikuwako Yerusalemi Wayahudi wakikaa, watu watawa, watu wa killa taifa chini ya uwingu. 6 Bassi sauti hii ilipokuja makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa killa mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake. 7 Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Si hawa wote wasemao Wagalilaya? 8 Imekuwaje bassi sisi kusikia killa mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo? 9 Waparthi na Wamedi na Waelamiti, nao wakaao Mesopotamia, Yahudi ua Kappadokia, Ponto na Asia, 10 Frugia na Pamfulia, Misri na pande za Libua karibu na Kurene, na Warumi wageni, Wayahudi na Waongofu, 11 Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa maneno yetu matendo makuu ya Mungu. 12 Wakashangaa wote wakaingiwa na mashaka, wakaambiana, Maana yake nini mambo haya? 13 Wengine walidhihaki, wakisema, Wamelewa kwa mvinyo mpya. 14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale edashara, akapaaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemi, jambo hili lijulike kwenu, mkasikilize maneno yangu. 15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana; 16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoel: 17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, Nitawamwagia watu wote Roho yangu, Na wana wenu na binti zenu watatabiri, Na vijana wenu wataona maono: Na wazee wenu wataota ndoto: 18 Na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wauawake Roho yangu, Nao watatabiri, 19 Nitatoa ajabu katika mbingu juu, Na ishara katika inchi chini, Damu na moto, na mvuke wa moshi: 20 Jua litageuka kuwa giza, Na mwezi kuwa damu, Kabla ya kuja ile siku ya Bwana Iliyo kuu, dhahiri. 21 Na itakuwa killa atakaeliitia jiua la Bwana ataokolewa. 22 Enyi waume wa Israeli, sikieni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua; 23 mtu huyu alitwaliwa nanyi kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake taugu zamani, nanyi mkamsulibisha kwa mikono mibaya, mkamwua: 24 Mungu akamfufua, akilegeza utungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao. 25 Maana Daud amtaja khabari zake, Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote, Kwa kuwa yuko mkono wangu wa kuume, nisitikisike. 26 Kwa hiyo moyo wangu ukapendezwa, ulimi wangu ukafurahi; Tena mwili wangu nao utakaa katika matumaini. 27 Kwa maana hutaniacha roho yangu katika kuzimu: Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu. 28 Umenifundisha njia ya uzima; Utanijaza furaha kwa uso wako. 29 Ndugu, mniwie radhi, niseme pasipo khofu mbele yenu khabari za baba yetu mkuu Daud, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hatta leo. 30 Bassi kwa kuwa nabii, akijua ya kuwa Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika uzao wa viuno vyake kwa jinsi ya kiwiliwili atamwinua Kristo, akae katika kiti chake cha enzi; yeye mwenyewe 31 akitangulia kuyaona haya, alitaja khabari za kufufuka kwake Kristo, ya kama roho yake haikuachwa katika kuzimu, wala mwili wake hankuona uharibifu, 32 Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake. 33 Bassi akiisha kupandishwa hatta mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia. 34 Maana Daud hakupanda mbinguni: bali yeye mwenyewe amesema, Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti mkono wangu wa kuume. 35 Hatta nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako. 36 Bassi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo. 37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe killa mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na watoto wenu, na watu wote walio mbali, na wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu. 40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. 41 Nao waliolipokea neno lake kwa furaha wakabatizwa: na siku ile wakazidishiwa watu wapata elfu tatu. 42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali. 43 Killa mtu akaingiwa na khofu: ajabu nyingi na ishara zikafanyika kwa ujumbe wa mitume. 44 Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika, 45 wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama killa mtu alivyokuwa na haja. 46 Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kupokea chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, 47 wakimsifu Mungu, na kuwapendeza wutu wote. Bwana akalizidisha kanisa killa siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania