Matendo 19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 IKAWA, Apollo alipokuwa Korintho, Paolo, akiisba kupita kati ya inchi za juu, akafika Efeso: akakutana na wanafunzi kadha wa kadba huko: 2 akawauliza, Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hatta kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. 3 Akawauliza, Bassi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana. 4 Paolo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakaekuja nyuma yake, yaani Kristo Yesu. 5 Waliposikia baya wakabatizwa katika jina la Bwana Yesu. 6 Na Paolo, alipokwisba kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri. 7 Na jumla yao walipata wanaume thenashara. 8 Akaingia ndani ya sunagogi, akanena kwa ujasiri, akihujiana na watu kwa muda wa miezi mitatu, na kuwavuta waamini mambo ya ufalme wa Mungu. 9 Lakini wengine walikaidi, wakakataa kuamini, wakiitukana ile Njia mbele ya mkutano; bassi, akaondoka akawaacha, akawatenga wanafunzi nao, akahujiana na watu killa siku katika darasa ya mtu mmoja, jina lake Tyranno. 10 Mambo haya yakaendelea kwa muda wa miaka miwili, hatta wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana, Wayahudi kwa Wayunani. 11 Mungu akafanya kwa mikono ya Paolo miujiza ya kupita kawaida; 12 hatta wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizogusa mwili wake, magonjwa yao yakawaondokea, pepo wachafu wakawatoka. 13 Baadhi ya Wayahudi wenye kutangatanga, nao ni waganga wa pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Twawaapizeni kwa Yesu, yule anaekhubiriwa na Paolo. 14 Nao waliofanya haya walikuwa wana saba wa Skewa, Myahudi, kuhani mkuu. 15 Yule pepo akawajibu, Yesu namjua na Paolo namfahamu, bali ninyi ni nani? 16 Na yule mtu aliyepagawa na pepo akawarukia, akawaweza, akawashinda, hatta wakatoka mbio katika nyumba ile uchi na wamejeruhi. 17 Khabari hii ikajulikana na Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, khofu ikawaingia wote, jina la Bwana Yesu likaadhimishwa. 18 Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama, wakidhihirisha matendo yao. 19 Na watu wengi katika wale waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote: wakafanya hesabu ya thamani yake wakaona ya kwamba yapata fedha khamsini elfu. 20 Hivyo neno la Mungu likazidi na kushinda kwa nguvu. 21 Mambo hayo yalipokwisha kumalizika, Paolo akaazimu rohoni mwake kupita kati ya Makedonia na Akaia aende Yerusalemi, akisema, Baada ya kuwako huko, yanipasa kuuona na Rumi. 22 Akatuma watu wawili miongoni mwa wale waliomkhudumia kwenda Makedonia, nao ni Timotheo na Erasto, yeye mwenyewe akakaa katika Asia kitambo. 23 Hatta wakati huo kukatukia ghasia si haba katika khabari ya Njia ile. 24 Kwa maana mtu mmoja, jina lake Demetrio, mfua fedha, kazi yake kufanya vihekalu vya fedha vya Artemi, alikuwa akiwapatia mafundi faida nyingi. 25 Akawakusanya hao, pamoja na wengine wenye kazi ile ile, akasema, Enyi wanaume, mnajua ya kuwa utajiri wetu hutoka katika kazi hii. 26 Tena mnaona na kusikia ya kwamba si katika Efeso tu, bali katika Asia yote pia, Paolo huyo amewaaminisha watu wengi na kuwageuza nia zao, akisema ya kwamba miungu inayofanywa kwa mikono siyo Mungu. 27 Si kwamba kazi hii yetu ina khatari ya kudharauliwa, bassi; bali na hekalu ya mungu mke aliye mkuu kuhesabiwa si kitu, na kuondolewa utukufu wake, ambae Asia yote pia na walimwengu wote humwtihudu. 28 Waliposikia haya wakajaa hasira, wakapiga kelele, wakisema, Artemi wa Waefeso m mkuu. 29 Mji wote ukajaa ghasia, wakaenda mbio wakaingia theatro kwa moyo mmoja, wakiisha kuwakamata Gaio na Aristarko, watu wa Makedonia waliosafiri pamoja na Paolo. 30 Na Paolo alipotaka kuingia kati ya watu, wanafunzi hawakumwacha aingie. 31 Walakini baadhi ya Waasiarko walio rafiki zake wakatuma watu kwake, wakimsihi asijihudhurishe nafsi yake ndani ya theatro. 32 Bassi wengine walikuwa wakilia hivi na wengine hivi: kwa maana ule mkutano umekwisha kuchafukachafuka, na walio wengi hawakuijua sababu ya kukusanyika kwao pamoja. 33 Wakatoa Iskander katika mkutano, Wayahudi wakimweka mbele ya watu. Iskander akawapungia mkono, akitaka kuwapa wale watu majibu. 34 Lakini walipotambua ya kuwa yeye ni Myahudi, wakapiga kelele wote pia kwa sauti moja kwa muda wa saa mbili au karibu, wakilia, Artemi wa Waefeso ni mkuu. 35 Na karani wa mji alipokwisha kuwatuliza watu, akasema, Enyi wanaume wa Efeso, ni mtu gani asiyejua ya kuwa mji wa Efeso ni mtunzaji wa hekalu ya Artemi, mungu mke aliye mkuu, na wa kitu kile kilichoanguka kutoka mbinguni? 36 Bassi kwa kuwa mambo haya hayawezi kukanushwa, imewapaseni kutulia, msifanye neno la haraka haraka. 37 Kwa maana mmewaleta watu hawa, wasiokwiba vitu vya hekalu wala kumtukana mungu mke wetu. 38 Bassi ikiwa Demetrio na mafundi walio pamoja nae wana neno juu ya mtu, baraza ziko, na maliwali wako: na washitakiane. 39 Bali mkitafuta neno lo lote katika mambo mengine, yatatengenezwa katika kusanyiko lililo halali. 40 Kwa maana tuna khatari ya kushtakiwa fitina kwa ajili ya mambo haya ya leo, ikiwa hakuna sababu ambayo kwa ajili yake tutaweza kujiudhuru kwa mkutano huu. 41 Alipokwisba kusema haya akauvunja mkutano. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania