Matendo 17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 WAKIISHA kupita kati ya Amfipoli na Apollonia wakafika Thessalonika, na hapo palikuwa na sunagogi la Wayahudi. 2 Na Paolo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahujiana nao kwa maneno yii maandiko sabato tatu, 3 akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kama, Yesu huyu ninaewapasha ninyi khabari zake ndiye Kristo. 4 Wengine wakaamini, wakasuhubiana na Paolo na Sila; na Wayunani waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye eheo si wachache. 5 Na Wayahudi wasioamini wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yason wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji; 6 na wasipowakuta, wakamkokota Yason na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika na huku, 7 Yason akawakaribisha; na hawa wote wanatenda mambo yaliyo kinyume cha amri za Kaisari, wakisema ya kwamba yupo mfalme mwingine, aitwae Yesu. 8 Wakautabarakisha nle mkutano na wakubwa wa mji walipoyasikia hayo. 9 Nao walipokwisha kumtoza dhamana Yason na wenziwe wakawaacha waende zao. 10 Marra ndugu wakawapeleka Paolo na Sila usiku hatta Beroya. Walipofika huko wakaingia katika sunagogi la Wayahudi. 11 Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thessaloniki, kwa kuwa walilipokea Neno kwa uelekefu wa moyo, wakayachunguza maandiko, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo. 12 Wafu wengi wakaamini miongoni mwao, nao wanawake wa Kiyunani wenye cheo, na wanaume si wachache. 13 Lakini Wayahudi wa Thessaloniki walipopata khabari ya kwamba Neno la Mungu linakhubiriwa na Paolo katika Beroya, wakaenda huko wakawachafua makutano. 14 Marra hiyo wale ndugu wakampeleka Paolo aende zake kana kwamba anakwenda njia ya pwani; bali Sila na Timotheo wakashinda huko. 15 Nao walimsindikiza Paolo wakampeleka hatta Athene; na wakiisha kupokea maagizo kuwapelekea Sila na Timotheo, ya kama wasikawie kumfuata, wakaenda zao. 16 Paolo alipokuwa akiwangojea katika Athene akaona jinsi mji ule ulivyojaa sanamu, roho yake ilichukizwa sana ndani yake. 17 Bassi katika sunagogi akahujiana na Wayahudi nao waliomcha Mungu, na killa siku sokoni na wale waliokutana nae. 18 Na baadhi ya Waepikurio na Wastoiko, matilosofo, wakakutana nae. Wengine wakasema, Mtu huyu mwenye maneno mengi anataka kusema nini? Wengine walisema, Anaonekana kuwa mtangaza khabari za miungu migeni, kwa maana alikuwa akikhubiri khabari za Yesu na ufufuo. 19 Wakamshika, wakamchukua hatta Areopago, wakisema, Je, twaweza kujua maana ya elimu hii mpya inenwayo nawe? 20 Kwa maana unaleta mambo mageni masikioni mwetu, tutapenda kujua, bassi, maana ya mambo haya. 21 Kwa maana Waathene na wageni waliokaa huko walikuwa hawana faragha kwa neno lo lote illa kutoa khabari na kusikiliza khabari za jambo jipya. 22 Paolo akasimaina katikati ya Areopago, tikasema, Enyi watu wa Athene, katika mambo yote naona ya kuwa ninyi ni watu wa kutafakari sana mambo ya dini. 23 Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona maabudu yenu, naliona madhliahu iliyoandikwa maneno haya, Kwa Mungu yule asiyejulikana. Bassi mimi nawakhubirini khabari zake yeye ambae ninyi mnamwabudu hila kumjua. 24 Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na inchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono: 25 wala hatumikiwi kwa mikono ya wana Adamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anaewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote. 26 Nae alifanya killa taifa ya wana Adamu kuwa wa damu moja, wakae juu ya uso wa inchi yote, akiisha kuwaandikia nyakati alizowaamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao; 27 illi wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasapapasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na killa mmoja wenu. 28 Kwa maana ndani yake tunaishi, tunakwenda, tuna uhayi wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi, alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake. 29 Bassi, kwa kuwa sisi tu wazao wa Mungu, haitupasi kudhani ya kuwa Uungu ni mfano wa dhahabu au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi na akili za wana Adamu. 30 Bassi zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hauoni; bali sasa anawakhuhiri watu wote wa killa mahali watubu. 31 Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa ujumbe wa mtu yule aliyemchagua; nae amewapa watu wote bayana ya mambo haya kwa kumfufua katika wafu. 32 Bassi waliposikia khabari za ufufuo wa wafu wengine wakadhihaki: wengine wakasema, Tutakusikiliza tena khabari hiyo. 33 Bassi Paolo akaondoka akawaacha. 34 Baadhi ya wanaume wakashikamana nae, wakaamini; katika hao alikuwamo Dionuso, Mwareopago, na mwanamke mmoja jina lake Damari, na watu wengine pamoja na hao. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania