Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 AKAFIKA Derbe na Lustra, na hapo palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, mwana wa mwanamke mmoja Myahudi aliyeamini: lakini baba yake alikuwa Myunani.

2 Mtu huyo alishuhudiwa na ndugu waliokaa Lustra na Derbe.

3 Paolo akamtaka huyu afuatane nae, akamtwaa akamtahiri kwa ajili ya Wayahudi waliokuwako pande zile: kwa maana wote walijua ya kuwa baba yake ni Myunani.

4 Bassi walipokuwa wakipita kati ya miji ile, wakawapa zile amri zilizoamriwa na mitume na wazee walioko Yerusalemi, illi wazishike.

5 Makanisa yakatiwa nguvu kwa imani, hesabu yao ikaongezeka killa siku.

6 Wakapita katika inchi ya Frugia na Galatia, wakakatazwa na Roho Mtakatifu, wasilikhubiri Neno katika Asia.

7 Walipofika kukabili Musia, wakajaribu kwenda Bithunia, lakini Roho ya Yesu hakuwapa rukhusa,

8 wakapita Musia wakatelemkia Troa.

9 Paolo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi akimwambia, Vuka uje Makedonia utusaidie.

10 Bassi alipokwisha kuona yale maono, marra tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Bwana ametuita tuwakhubiri Injili.

11 Tukangʼoa nanga kutoka Troa, tukafika Samothraki kwa tanga moja.

12 Siku ya pili tukafika Neapoli na kutoka hapo tukafika Filippi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika wilaya ile, nayo ni Kolonia ya Kirumi; tukawa katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha.

13 Hatta siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, tukidhani ya kuwa hapo pana mahali pii kuomba; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale.

14 Mwanamke mnioja, jina lake Ludia, mwenye kuuza rangi ya zambarao, mwenyeji wa Thuatira, mcha Mungu, akatusikiliza. Moyo wake huyu ukafunguliwa na Bwana, ayaangalie mineno yaliyonenwa na Paolo.

15 Hatta alipokwisha kumbatiza, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae; akatushurutisha.

16 Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kuombea, kijakazi kimoja aliyekuwa na pepo ya Puthoni akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kutabiri.

17 Akamfuata Paolo na sisi, akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kutukhubiri njia ya wokofu.

18 Akawa akifanya hayo siku nyingi. Lakini Paolo akakasirika akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.

19 Bassi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paolo na Sila, wakawakokota hatta sokoni mbele ya wakuu wa mji;

20 wakawachukua kwa makadhi, wakasema, Watu hawa wanataharakisha mji wetu, nao ni Wayahudi.

21 Tena wanatangaza khabari ya desturi zisizo halali kwetu tuzipokee wala kuzifuata, kwa kuwa sisi tu Warumi.

22 Makutano wote wakaondoka wakawaendea, Makadhi wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora.

23 Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana.

24 Nae akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale.

25 Lakini panapo usiku wa manane Paolo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakisikiliza.

26 Ghafula pakawa tetemeko kuu la inchi, hatta misingi ya gereza ikatikisika, na marra hiyo milango ikafunguka, vifungo vya watu wote vikalegezwa.

27 Yule mlinzi wa gereza akaamka, akaona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, akafuta upanga wake, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia.

28 Paolo akapaaza sauti yake kwa uguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa.

29 Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa khofu, akawaangukia miguu Paolo na Sila;

30 kiisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, nifanye nini nipate kuokoka?

31 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka pamoja na uyumba yako.

32 Wakamwambia neno la Bwana, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake.

33 Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, akahatizwa, yeye ua watu wote wa nyumbani mwake wakati huohuo.

34 Akawaleta juu nyumbani kwake, akawaandalia, akafurahi sana, yeye na nyumba yake yote, maana amekwisha kumwamini Mungu.

35 Kulipopambazuka makadhi wakawatuma wakubwa wa askari wakisema, Waacheni watu wale waende zao.

36 Yule mlinzi wa gereza akamwarifu Paolo maneno haya ya kama, Makadhi wametuma watu kuwafungulieni! bassi, sasa tokeni nje, enendeni zenu kwa amani.

37 Paolo akawaambia, Wametupiga mbele ya watu wote bila kutuhukumu, na sisi tu Warumi, teua wametutupa gerezani; na sasa wanataka kututoa kwa siri? la, sivyo, na waje wenyewe wakatutoe.

38 Wakubwa wa askari wakawapasha makadhi khabari za maneno haya: nao wakaogopa, waliposikia ya kwamba ni Warumi.

39 Wakaja wakawasihi: na walipokwisha kuwatoa nje, wakawaomba watoke katika mji ule.

40 Nao wakatoka gerezani wakaingia nyumbani mwa Ludia; na walipokwisha kuwaona ndugu wakawafariji, wakaenda zao.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo