Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 WAKASHUKA wafu waliotoka Yahudi wakawafundisha ndugu ya kama, Msipotahiriwa na kuifuata desturi ya Musa hamwezi kuokoka.

2 Bassi baada ya Paolo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhujiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paolo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemi kwa mitume na wazee kwa khabari ya swali hilo.

3 Bassi, wakisafirishwa na Kanisa, wakapita kati ya inchi ya Foiniki na Samaria, wakitangaza khabari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana.

4 Walipofika Yerusalemi wakakaribishwa na Kanisa na mitume na wazee, nao wakawaeleza mambo yote Mungu aliyoyafanya pamoja nao.

5 Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika Torati ya Musa.

6 Mitume na wazee wakakusanyika wapate kulifikiri neno hilo.

7 Na baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya kuwa siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwetu mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini.

8 Na Mungu, ajuae mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vilevile kama alivyotupa sisi;

9 wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani.

10 Bassi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka nira juu ya shingo za wanafunzi, ambayo baba zetu na sisi hatukuweza kuichukua.

11 Bali twaamini kwamba kwa neema ya Bwana Yesu tutaokoka kama wao.

12 Bassi mkutano wote wakanyamaza, wakawasikiliza Barnaba na Paolo wakiwapasha khabari za ishara na maajabu ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika mataifa.

13 Na bao walipokwisha kunyamaza Yakobo akajibu, akinena, Ndugu zangu, nisikilizeni,

14 Simeon ametueleza jinsi Mungu alivyowaangalia mataifa illi achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake.

15 Na maneno ya manabii yapatana na bayo, kama ilivyoandikwa:

16 Baada ya mambo haya nitarejea, Nami nitaijenga tena nyumba ya Daud iliyoanguka. Nitajenga tena maanguko yake, Na nitaisimamisha;

17 Illi wana Adamu waliosalia wamtafute Bwana, Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa kwao: Asema Bwana afanyae mambo haya yote.

18 Kazi zake zote zimejulika na Mungu tangu mwanzo wa ulimwengu.

19 Kwa sababu hiyo mimi naamua hivi: Tusiwataabishe wale waliomgeukia Mungu katika Mataifa:

20 balituwaandikie wajiepushe na unajisi wa sanamu na asharati na nyama zilizosongwa na damu.

21 Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wakhubirio mambo yake; katika killa mji husomwa killa siku katika masunagogi.

22 Bassi ikawapendeza mitume na wazee na Kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwapeleka Antiokia pamoja na Paolo na Barnaba: nao ni hawa, Yuda aliyekwitwa Barsaba, na Sila, watu wakuu katika ndugu.

23 Wakaandika hivi kwa mikono yao, Mitume na wazee na ndugu, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shami na Kilikia, walio wa mataifa, salamu.

24 Kwa kuwa tumesikia ya kwamba watu waliotoka kwetu wamewasumbueni kwa maneno yao, wakipotosha roho zenu, wakisema, ya kuwa hamna buddi kutahiriwa na kuishika Torati, ambao sisi hatukuwapa agizo lo lote;

25 bassi tumeona vema tukiwa tumepatana kwa moyo mmoja, kuwachagua watu na kuwapeleka kwenu pamoja na wapendwa wetu Barnaba na Paolo,

26 watu waliokhatirisha maisha zao kwa ajili ya jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

27 Bassi tumewatuma Yuda na Sila, watakaowaambieni maneno yayo hayo kwa vinywa vyao.

28 Kwa maana ilimpendeza Roho Mtakatifu na sisi, tusiwatwike mzigo illa hayo yaliyo faradhi,

29 mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongwa, na asharati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Salamu.

30 Hatta hao wakiisha kupewa rukhusa wakatelemkia Antiokia; na baada ya kuwakusanya jamii yote wakawapa ule waraka.

31 Wakausoma, wakafurahi kwa ajili ya faraja ile.

32 Tena Yuda na Sila, kwa kuwa wao wenyewe ni manabii, wakawausia ndugu kwa maneno mengi, wakawathubutisha.

33 Nao wakiisha kukaa huko muda kitambo, wakarukhusiwa na ndugu waende kwa amani kwao waliowatuma.

34 Lakini Sila akaona vema kukaa huko.

35 Na Paolo na Barnaba wakakaa huko Antiokia, wakifundisiia na kulikhubiri neno la Bwana, pamoja na watu wengine wengi.

36 Baada ya siku kadha wa kadha Paolo akamwambia Barnaba, Haya! turejee sasa tukawaangalie ndugu katika killa mji tulipolikhubiri neno la Bwana, wa hali gani.

37 Barnaba akaazimu kumchukua Yohana aliyekwitwa Marko pamoja nao.

38 Bali Paolo hakuona vema kumchukua huyo aliyewaacha huko Pamfulia, asiende nao kutenda ile kazi.

39 Bassi palitokea maneno makali beina yao hatta wakatengana: Barnaba akamchukua Marko akatweka kwenda Kupro.

40 Paolo akamchagua Sila akaondoka, akiombewa na wale ndugu, apewe neema ya Mungu.

41 Akapita katika Shami na Kilikia akawatia moyo makanisa.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo